Simba yamsajili Ayoub Lakred kutoka FA Rabat

Simba yamsajili Ayoub Lakred kutoka FA Rabat

Charmaine

Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
61
Reaction score
161
842b547a-d70c-4129-b029-a3409de01dd2.jpg


Kipa mwenye Level za Kimataifa ambae amecheza Mashindano yote makubwa Africa yaani Champions League na mwaka Jana Timu yake imefika Nusu Fainali ya Confederation Cup hapa utawataja FAR RABAT ambao msimu huu ulioisha ndio Mabingwa wa Ligi Morocco.

AYOUB LAKRED ni Raia wa Morocco ambae amechezea Timu ya Taifa ya Morocco mechi mbalimbali pamoja na CHAN ni kipa kiongozi ambae ana umri halisi wa miaka 28 sasa zamani alichezea RS BERKANE kabla ya kuchukuliwa na FAR Rabat zote za Morocco.

AYOUB LAKRED ambae alikuwa na Mkataba unaishia June 2025 pale FAR RABAT amejiunga na Simba Sports Club kwa mkataba wa miaka miwili toka sasa anakwenda kusaidiana na Ally Salim na Hussein Abel pamoja na kinda aliepandishwa kutoka U20 kupata Uzoefu Ahmed Feruzi kipindi hiki ambacho Kipa namba moja Aishi Manula anakiendelea kuuguza Majeraha yake chini ya kitaalam wetu.

AYOUB LAKRED NI MNYAMA
 
Nimemuona. Licha ya kuzuia hatari kubwa kubwa, kipa huyu anapiga pasi za mguu utadhani kiungo mchezeshaji
 
Kwa usajili huu halafu mfanye vibaya ndani na nje nadhani MTAFARAKANA SANA
 
Hongera mtani

Sajili vizuri tushindane kiwanjani
 
Game ya kesho lawama zote zitatupiwa kwa kipa, ili kuzima soo after game ya kesho imebidi leo atambulishwe kipa.
 
Game ya kesho lawama zote zitatupiwa kwa kipa, ili kuzima soo after game ya kesho imebidi leo atambulishwe kipa.
Kwa hiyo Simba wameingia gharama ya mamilioni kumsajili huyo golikipa ili kuzima soo la kufikirika?

Utopolo wengi kichwani kuna ubongo wenye 4kB
 
Game ya kesho lawama zote zitatupiwa kwa kipa, ili kuzima soo after game ya kesho imebidi leo atambulishwe kipa.
Kwani ile tuliyowakanda mbili kabla ya game tulimtambulisha nani? Au hakuwa Ally Salim yule?
 
Huyo sasa ni golikipa sio mlinda mlango
 
Back
Top Bottom