Charmaine
Member
- Jan 4, 2023
- 61
- 161
Kipa mwenye Level za Kimataifa ambae amecheza Mashindano yote makubwa Africa yaani Champions League na mwaka Jana Timu yake imefika Nusu Fainali ya Confederation Cup hapa utawataja FAR RABAT ambao msimu huu ulioisha ndio Mabingwa wa Ligi Morocco.
AYOUB LAKRED ni Raia wa Morocco ambae amechezea Timu ya Taifa ya Morocco mechi mbalimbali pamoja na CHAN ni kipa kiongozi ambae ana umri halisi wa miaka 28 sasa zamani alichezea RS BERKANE kabla ya kuchukuliwa na FAR Rabat zote za Morocco.
AYOUB LAKRED ambae alikuwa na Mkataba unaishia June 2025 pale FAR RABAT amejiunga na Simba Sports Club kwa mkataba wa miaka miwili toka sasa anakwenda kusaidiana na Ally Salim na Hussein Abel pamoja na kinda aliepandishwa kutoka U20 kupata Uzoefu Ahmed Feruzi kipindi hiki ambacho Kipa namba moja Aishi Manula anakiendelea kuuguza Majeraha yake chini ya kitaalam wetu.
AYOUB LAKRED NI MNYAMA