Simba yamtangaza Zubeda Sakuru kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu (CEO) mpya wa klabu

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Screenshot_2024_11_23_16_57_21_579_com_instagram_android_edit.jpg
Tunapenda kuutarifu umma kuwa Klabu ya Simba, imefikia makubaliano ya kusitisha mkataba na Ndugu Francois Regis, ambaye alikuwa ni Mtendaji Mkuu kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu. Tunamshukuru Mr. Regis kwa kipindi alichohudumu katika Klabu yetu.

Bodi imefanya uteuzi wa Bi. Zubeda Hassan Sakuru kama Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mkuu.

Bi. Zubeda yuko mbioni kuhitimu Shahada yake ya Kwanza ya Uzamivu, ana Shahada mbili za Uzamili katika Utawala wa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Warwick, Uingereza na Chuo Kikuu cha Mzumbe Tanzania. Pia ana Shahada ya Kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe.

Bi. Zubeda amefanya kazi kama Meneja Miradi wa Simba akimsaidia Bw. Kajula kuhusu mchakato wa kutengeneza sera na ushauri wa masuala ya kiutendaji.

Tafadhali ungana nasi kumtakia heri Regis na kumkaribisha Zubeda katika Klabu ya Simba.

PIA SOMA
- Simba wamtangaza CEO mpya, mrithi wa Imani Kajula
 
Naona kama tuna uhaba wa wataalamu waliosomea masuala ya utawala katika michezo. Nadhani wengi bado hawajaona hiyo fursa.

Huyu bidada elimu yake haihusiani kabisa na masuala ya michezo na hata pilikapilika zake inaonyesha hakuwa anajichanganya kwenye workshops za masuala ya utawala wa michezo. Inaonyesha hakuwa na mpango sana na eneo hilo.

Najua kama ana IQ nzuri na ni mshabiki mzuri wa soka, haraka tu ataweza kujijenga kiufahamu kwenye masuala muhimu ya utawala wa soka. Wasiwasi wangu asije tu akawa Kajula mwingine aliyejikita katika masuala ya marketing huku timu inaporomoka.
 
CEO msaidizi huyu atakuwa ana hudumia wafanyakazi pamoja na wachezaji, bila kusahau miradi ya simba

To manage business and people
 
Huyo siyo CEO msaidizi, bali ni CEO mwenyewe. Kwenye mpira unahitaji kiongozi ambaye ana passion na mpira na pilikapilika zake. Simba inahitaji mtu aliye na njaa na kiu na mafanikio ya timu uwanjani siyo tu kuhudumia wafanyakazi na miradi. Inahitaji mtu asiyependa kushindwa siyo mpita njia au anayeangalia fursa binafsi (type ya kina Salim Abdallah na Mangungu).

Kwa sasa nampa benefit of a doubt.
 
Tunapenda kuutarifu umma kuwa Klabu ya Simba, imefikia makubaliano ya kusitisha mkataba na Ndugu Francois Regis, ambaye alikuwa ni Mtendaji Mkuu kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu. Tunamshukuru Mr. Regis kwa kipindi alichohudumu katika Klabu yetu.

Bodi imefanya uteuzi wa Bi. Zubeda Hassan Sakuru kama Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mkuu.

Bi. Zubeda yuko mbioni kuhitimu Shahada yake ya Kwanza ya Uzamivu, ana Shahada mbili za Uzamili katika Utawala wa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Warwick, Uingereza na Chuo Kikuu cha Mzumbe Tanzania. Pia ana Shahada ya Kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe.

Bi. Zubeda amefanya kazi kama Meneja Miradi wa Simba akimsaidia Bw. Kajula kuhusu mchakato wa kutengeneza sera na ushauri wa masuala ya kiutendaji.

Tafadhali ungana nasi kumtakia heri Regis na kumkaribisha Zubeda katika Klabu ya Simba.

PIA SOMA
- Simba wamtangaza CEO mpya, mrithi wa Imani Kajula
Anafaa sana.
Cc Engonga
 
CV ÿa kaimu CEO imeshiba sio haba. Sasa tunasubiri utemdaji kazi wake utasadifu yaliyomo kwenye makaratasi
 
Tunapenda kuutarifu umma kuwa Klabu ya Simba, imefikia makubaliano ya kusitisha mkataba na Ndugu Francois Regis, ambaye alikuwa ni Mtendaji Mkuu kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu. Tunamshukuru Mr. Regis kwa kipindi alichohudumu katika Klabu yetu.

Bodi imefanya uteuzi wa Bi. Zubeda Hassan Sakuru kama Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mkuu.

Bi. Zubeda yuko mbioni kuhitimu Shahada yake ya Kwanza ya Uzamivu, ana Shahada mbili za Uzamili katika Utawala wa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Warwick, Uingereza na Chuo Kikuu cha Mzumbe Tanzania. Pia ana Shahada ya Kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe.

Bi. Zubeda amefanya kazi kama Meneja Miradi wa Simba akimsaidia Bw. Kajula kuhusu mchakato wa kutengeneza sera na ushauri wa masuala ya kiutendaji.

Tafadhali ungana nasi kumtakia heri Regis na kumkaribisha Zubeda katika Klabu ya Simba.

PIA SOMA
- Simba wamtangaza CEO mpya, mrithi wa Imani Kajula
Zubeda FC
 
Back
Top Bottom