Simba yamtangaza Zubeda Sakuru kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu (CEO) mpya wa klabu

Simba yamtangaza Zubeda Sakuru kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu (CEO) mpya wa klabu

Mentor wangu ana degree moja na aliniambia hivyo hivyo.

Degree ya kwanza inatosha.
Inategemea una ndoto za kuwa nani. Kama upo kwenye soko la kuajiriwa halafu unakomaa na degree moja, ndugu yangu utachelewa sana. Mfano kazi kama za World Bank bila Masters hutoboi.

Mimi nilikuwa nina akili kama yako lakini nikaja kwenye conclusion kwamba ni bora kuongeza tu elimu. We kama unajiona una akili just demonstrate kwenye vyeti, acha ile habari ya kujiona una akili. Stroke
 
Tunapenda kuutarifu umma kuwa Klabu ya Simba, imefikia makubaliano ya kusitisha mkataba na Ndugu Francois Regis, ambaye alikuwa ni Mtendaji Mkuu kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu. Tunamshukuru Mr. Regis kwa kipindi alichohudumu katika Klabu yetu.

Bodi imefanya uteuzi wa Bi. Zubeda Hassan Sakuru kama Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mkuu.

Bi. Zubeda yuko mbioni kuhitimu Shahada yake ya Kwanza ya Uzamivu, ana Shahada mbili za Uzamili katika Utawala wa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Warwick, Uingereza na Chuo Kikuu cha Mzumbe Tanzania. Pia ana Shahada ya Kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe.

Bi. Zubeda amefanya kazi kama Meneja Miradi wa Simba akimsaidia Bw. Kajula kuhusu mchakato wa kutengeneza sera na ushauri wa masuala ya kiutendaji.

Tafadhali ungana nasi kumtakia heri Regis na kumkaribisha Zubeda katika Klabu ya Simba.

PIA SOMA
- Simba wamtangaza CEO mpya, mrithi wa Imani Kajula
CEO wa ule mtaa mwingine ana degree gani vile?
 
Ameolewa?

Nadhani watu walioimudu vizuri sana Simba ni Senzo pamoja na Barbara. Kajula alikuwa mbabaishaji tu. SImba wangefanya busara wamwangukie Barbara tena na kumlamba miguu wakimwomba msamaha ili awanusuru na mzigo unaowaelemea sasa.

Hata hivyo, kwa adui wako kukiwaka moto, wewe peleka petroli, usipeleke maji ila mimi nimewapelekea maji.
 
Bora aisee maana ataacha kuuza vitafunwa. Alikua anajua sana kupika sambusa na maandazi
 
Zubeda aliwahi kuwa mbunge wa CDM?
Alibebwa kilazima akapitishwa kilazima na mwenyekiti, watu waliandamana Ila mwenyekiti akakaza. Maswali yakaibuka...

Mwenyekiti nae akazungukwa, 2020 akasema kila mbunge wa viti maalum ni lazima atafute Jimbo agombee, zubby siasa hajui asingeweza kugombea popote akaachana na siasa, akapata shavu kusoma uk kupitia chevening. Baadae akahama chama
 
Huyu Zubeda Sakuru Alikuwa Mbunge wa Chadema, Then na Baba yake Mzazi Alichezea SIMBA, Brother Sakuru, Kwa hiyo huyo Sio Simba mbugirambugira huyo Simba Damu KABISA, Mzee Sakuru kachezea Sunderland Baadaye Akachezea Simba sports club
Usiwaamini sana wanawake, huyo kuna kipindi hapa katikati alikua yanga.
 
Back
Top Bottom