Simba yamtangaza Zubeda Sakuru kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu (CEO) mpya wa klabu

Simba yamtangaza Zubeda Sakuru kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu (CEO) mpya wa klabu

Naona kama tuna uhaba wa wataalamu waliosomea masuala ya utawala katika michezo. Nadhani wengi bado hawajaona hiyo fursa.

Huyu bidada elimu yake haihusiani kabisa na masuala ya michezo na hata pilikapilika zake inaonyesha hakuwa anajichanganya kwenye workshops za masuala ya utawala wa michezo. Inaonyesha hakuwa na mpango sana na eneo hilo.

Najua kama ana IQ nzuri na ni mshabiki mzuri wa soka, haraka tu ataweza kujijenga kiufahamu kwenye masuala muhimu ya utawala wa soka. Wasiwasi wangu asije tu akawa Kajula mwingine aliyejikita katika masuala ya marketing huku timu inaporomoka.
Yule Kajula alikua ni pure Afisa masoko..Madili mapya kila siku huku timu ikiwa inazama shimoni😂
 
Hii karne ya 21 mnaajiri mtu kwa kuangalia vyeti?

Ukiona mtu ana degree nyibgi nyingi ujue huyo ni dhaifu hajiamini
Kwamba specialist wa ubongo hajiamini? Maana hiyo taaluma unasoma mno. Au unasemea hizi degree za biashara,uhasibu na masoko sijui procure?
 
Hii karne ya 21 mnaajiri mtu kwa kuangalia vyeti?

Ukiona mtu ana degree nyibgi nyingi ujue huyo ni dhaifu hajiamini
Mentor wangu ana degree moja na aliniambia hivyo hivyo.

Degree ya kwanza inatosha.
 
Tunapenda kuutarifu umma kuwa Klabu ya Simba, imefikia makubaliano ya kusitisha mkataba na Ndugu Francois Regis, ambaye alikuwa ni Mtendaji Mkuu kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu. Tunamshukuru Mr. Regis kwa kipindi alichohudumu katika Klabu yetu.

Bodi imefanya uteuzi wa Bi. Zubeda Hassan Sakuru kama Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mkuu.

Bi. Zubeda yuko mbioni kuhitimu Shahada yake ya Kwanza ya Uzamivu, ana Shahada mbili za Uzamili katika Utawala wa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Warwick, Uingereza na Chuo Kikuu cha Mzumbe Tanzania. Pia ana Shahada ya Kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe.

Bi. Zubeda amefanya kazi kama Meneja Miradi wa Simba akimsaidia Bw. Kajula kuhusu mchakato wa kutengeneza sera na ushauri wa masuala ya kiutendaji.

Tafadhali ungana nasi kumtakia heri Regis na kumkaribisha Zubeda katika Klabu ya Simba.

PIA SOMA
- Simba wamtangaza CEO mpya, mrithi wa Imani Kajula
Warembo huwa wanakula shavu sana simba.
 
Screenshot_20241123-212638_Chrome.jpg

OKW BOBAN SUNZU
ngara23
Mbaga Jr
GENTAMYCINE
Nifah
chiembe
johnthebaptist
ChoiceVariable
Tlaatlaah
MamaSamia2025
Erythrocyte
 
Mbowe alijipakulia, Ila bungeni deep pocket theory ikatumika, Mbowe akapigwa chini, aliyembeba ndiyo yuko bize kumsomesha kama njia ya "kumficha" Mabazazi wasimuone, basi unafikiri anasomaaaaa? Walaaaa!, anaungaunga vyeti, kama alisoma basi ni form six ambako wanaomsahihisha mitihani hawamuoni
Ila wewe naye una mengi? Haya, aliyembeba ndio nani?
 
Mkuu umeona usiache lipite hadi ukafukue makaburi? Mbona nimesikia sifa zake yuko vizuri tu?
Tumpe nafasi, kisha tumpime kwa utendaji wake.
Screenshot_2024_11_23_16_57_21_579_com_instagram_android_edit.jpg


ZUBEDA ana shahada mbili za uzamili katika utawala wa umma kutoka chuo kikuu Mzumbe na chuo kikuu Warwick.

Hii ilikuwa ni joint degree au program? Au alipendelea kurisiti ulaya?

Au sijaelewa vizuri?
 
View attachment 3159857

ZUBEDA ana shahada mbili za uzamili katika utawala wa umma kutoka chuo kikuu Mzumbe na chuo kikuu Warwick.

Hii ilikuwa ni joint degree au program? Au alipendelea kurisiti ulaya?

Au sijaelewa vizuri?
Sijaelewa kwanini Simba wameweka kipaumbele cha elimu yake katika utambulisho wake badala ya uzoefu wake, ila tuachane na hilo kama nilivyosema tumpe nafasi kisha tumpime kwa utendaji wake.
 
Back
Top Bottom