Orketeemi
JF-Expert Member
- Feb 12, 2013
- 5,063
- 12,866
Mkuu...Kuna kipindi Yanga ilienda kuweka Kambi Moshi ikashindwa kulipia hoteli wakawa wanadaiwa hadi kushikiliwa gari lao
Labda uwe mgeni wa soka la simba na Yanga
Hizi timu hua migogoro inahama toka upande mmoja kwenda mwingine
Kabla ya Manji ...Yanga kuna wakati ilikua inalia njaa
Jumatano, 28 Desemba 2011
WACHEZAJI YANGA NJAA KALI, PESA HAKUNA.
Wachezaji Yanga walia njaa
![]()
Timu ya YangaIkiwa inakabiliwa na ushindani mkali katika kampeni yake ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na pia mashindano ya Klabu Bingwa Afrika, programu za mazoezi ya Yanga inashindwa kutekelezeka kikamilifu kutokana na wachezaji wake kutopata mishahara yao ya miezi miwili.Mishahara hiyo ambayo wachezaji wanadai ni ya mwezi Novemba na Desemba, ambao umeambatana na sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya.
Kwa mujibu wa habari ambazo gazeti hili imezipata ni kwamba mbali na wachezaji hao, pia wafanyakazi wengine walioajiriwa na klabu hiyo hawajalipwa kwa muda wa miezi mitatu sasa.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa hali hiyo ya ukata imechangia mambo mengi kutofanyika kama ilivyotarajiwa ikiwemo kuvurugika kwa programu ya mazoezi.
"Hali ni mbaya, klabu haina pesa, mambo mengi hayafanyiki kama ilivyokusudiwa, tunajaribu kufanya kila linalowezekana ili kutatua tatizo hili linalotukabili," alisema mmoja wa viongozi wa Yanga ambaye hakutaka jina lake litajwe.
Aliongeza kuwa kukosekana kwa fedha kutoka kwa aliyekuwa mfadhili wao na mapato madogo ya mlangoni yaliyokuwa yakipatikana katika mechi za mzunguko wa kwanza wa ligi ndio sababu nyingine iliyofanya klabu yao ikose fedha za kujiendesha.
Mambo yaliyonipa raha kwenye hiyo habari uliyoleta
1. Yanga ni ya kimataifa kitambo kumbe
2. Wapo wachezaji walikuwa first eleven 2011 mpaka leo wapo first elven duh