Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Kama unakumbuka sakata la Oktoba 25, 2023 la kukamatwa Makontena yenye jezi feki za klabu za Simba, Yanga, Azam na Timu ya taifa zilizoingia kimagendo nchini.
Wanahabari walikurupushwa usiku wakati wa ukamataji makontena hayo huku Afisa Habari wa Klabu ya Yanga Ally Kamwe akiwa mstari wa mbele katika ukamataji huo lakini tangu siku ile kumekuwa na ukimya na swali likabaki sakata hilo liliishia wapi?
Sasa kwa mujibu wa Tume ya Ushindani (FCC) ni kwamba yalikuwa mashehena manne yaliyojaa jezi feki ambazo ziliingia kimagendo.
Mkurugenzi wa udhibiti wa Bidhaa Bandia kutoka Tume ya Ushindani FCC Bi. Khadija Ngasongwa, alisema baada ya kupokea taarifa hiyo walifika eneo la tukio na kubaini makontena hayo yalijaa jezi zisizo halisi za Yanga sc, Simba sc, Azam Fc na Taifa Stars ambayo pia yaliingia kimagendo bila kulipiwa kodi TRA.
Hata hivyo, baada ya tukio la kukamata TRA waliingilia kati wakalipwa kodi yao ya hizo kontena, Azam fc wao wakasema jezi zao ziteketezwe zikachomwa moto, wakati Yanga sc, Simba sc na TFF walikaa mezani na mtu aliyeingiza hizo jezi feki wakataka walipwe faida ambayo wangeweza kuipata kwenye mauzo ya hizo jezi kama zingekuwa za kwao na wakalipwa.
Je, kwanini jambo hili lilifanyika kwa usiri? na kwanini Yanga sc, Simba sc na TFF wakubali kulipwa faida ya mauzo ya jezi feki na kuruhusu kuingia sokoni? Je, mapato ya mgao waliopata ilishawahi kutolewa taarifa kwa wanachama wao?