Simba, Yanga waanza safari kuelekea Angola na Botswana kwa michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika

Simba, Yanga waanza safari kuelekea Angola na Botswana kwa michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Baada ya kumalizana na mchezo wa Ngao ya Jamii, vikosi vya Simba na Yanga, vimeanza safari kuelekea kwenye michezo yao ya Kimataifa katika nchi tofauti.

1758099973636.png
Kikosi cha Yanga kimeondoka alfajiri ya leo Jumatano Septemba 17, 2025 Dar es Salaam kuelekea Angola kwa ajili ya mchezo wa Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wiliete ya nchini humo, mchezo utakaochezwa Septemba 19, 2025 kwenye Uwanja wa Novemba 11, Luanda.

Simba wao wameanza safari kwenda Botswana kuvaana na Gaborone United ya nchini humo katika mechi ya raundi ya kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika itakayochezwa Jumamosi Septemba 20, 2025.

1758099891205.png
 
My wetu simba angesubiri kwanza maumivu yaishe.

Hata uchungu wa kupigwa kimoko cha jogoo hayajaisha washaanza visafari vya hapa na pale.
 
Wananchi Young Africans muwe na safari njema, na siku ya mechi hakikisheni mnawaangushia kichapo cha mbwa koko hao Waangola.
 
Binafsi niwe tu mkweli Sina shaka kabisa na kikosi Cha yanga lakini mashaka yangu yapo katika benchi la ufundi
 
Back
Top Bottom