Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 2,818
- 7,940
Nimewai kusoma kitabu cha ‘War Made Easy: How Presidents and Pundits Keep Spinning Us to Death’ kitabu kimeandikwa mwaka (2005) na Norman Solomon.
Moja ya mstari katika kitabu icho unasema “..., (he) alleges that many government administrations have distorted facts and manipulated the media to sell the necessity of war to the American people.”
Mwandishi ametumia mifano halisi kutoka vita ya Vietnam na Iraq dhidi ya Marekani jinsi filamu za kikomando zilizotengenezwa marekani Hollywood zilivyotumika kuogopesha maadui wa marekani, wewe umekaa zako kwenye TV unamuangalia Rambo akipigana na Wavietnam unafurahia kumbe wenzako hapo wanaeneza propaganda za kivita hili waogopwe, unamuangalia Arnold Schwerzenegge, unamuangalia Chock Norris, Van Damme, na Komando Kipensi na makomando wengineo unaona raha, wenzako wapo kazini mpaka leo Duniani watu wanaona Jeshi bora ni marekani kutokana na movie zilizotolewa. Media kama TV, Radio na Magazeti vilitumika sana kueneza propaganda na wamarekani kuwashida maadui. Yani serikali inaweza kuamua sasa hivi TV au mitandao ya kijamii izungumzie nini au kitu gani kitrendi kukwepesha wananchi wasizungumzie kitu fulani, mbatolewa kwenye uwepo mliopo mnapelekwa kwingine.
Sasa pia hiki kitabu nilichokibainisha hapo juu kuna filamu yake pia ilitengenezwa kwa jina hilo mwaka 2007..
Filamu imetayarishwa na Alper na kusimuliwa na Sean Penn. Ilionyeshwa kwa mara ya kwanza New York Mei 14, 2007, kabla ya kutolewa Agosti 24, 2007.
Filamu hiyo inajaribu kufichua jinsi serikali ya Marekani kwa zaidi ya miaka 50 imejaribu kuchochea juhudi za vita kwa kutumia vyombo vya habari kama chombo cha kubadilishia upepo wa vuguvugu za kisiasa duniani au vita.
Kwa hapa kwetu Bongonyoso, mambo yapo katika mapigo tofauti japo uzito wa ngumi ni ulele.
Sasa hivi kuna vuguvugu za kisiasa ambapo wananchi wanaotaka mabadiliko na vyama pinzani kama Chadema wamekuja na ajenda ya No reform, No election wakidai mabadiliko ya katiba itakayoruhusu uhuru katoka uchaguzi na mambo mengineyo.
Na Wakati huo huo timu ya Yanga imeleta mgomo wa kutokucheza ikishinikiza bodi ya ligi na shirikisho kufuata sheria na kanuni na viongozi kujiuzulu huku wakiwa na kauli mbiu 'Hatuchezi'. Simba nae akilalamika kuhusu yanga kuzuia mabasi ya wachezaji wake wasiingie uwanjani kuafanya mazoezi ya mwisho kabla ya derby
Hatuchezi na No Reform No Election ni kama zimepamba moto katika kipindi hiki. Ingawa, HATUCHEZI ya Young Africans SC na NO REFORMS, NO ELECTION zinaweza kuwa na muktadha sawa, lakini hii ya Yanga tuipime katika mizani…
Pamoja na kwamba Young Africans SC wanayo hoja ya msingi katika jambo lao, lakini wanaweza kutumika kufifisha mjadala wa “NO REFORMS; NO ELECTION”.
Hili linawezekana. Haji Manara amewahi kutueleza vizuri. Kwamba, Serikali ikiona maji yamekorogeka sana, wanazitumia Simba na Yanga kuhamisha mijadala
Manara anasema, utani wa Simba na Yanga unaleta utulivu kwenye siasa na Serikali inaunga mkono utani wa Simba na Yanga wakati maji, umeme, sukari hakuna.
Ukizingatia, viongozi wa Young Africans SC wote hadi wasemaji wake ni wanachama kindakindaki wa CCM na hata Mkutano Mkuu wa CCM, Dodoma, wamehudhuria.
Nimekumbuka ile nadharia maarufu ya iliyotumika mwaka 1968 inaitwa ‘Agenda—setting theory’ ambayo ilikuwa developed na Max McCombs and Donald Shaw.
Hii nadharia ilitumika kuendesha propaganda katika uchaguzi mkuu wa Marekani mwaka 1968, uchaguzi ambao Richard Nixon alimshinda Hubert Humphrey.
Mashabiki wa Yanga mnaopenda mabadiliko ya kisiasa katika nchi yetu, mliendee jambo hilo kwa tahadhari kubwa sana. Msikubali kuuziwa mbuzi kwenye gunia.
Msikubali kuhamishwa katika mjadala mkubwa wa kitaifa ambao unahusu mageuzi ya kimfumo katika sheria na kanuni za kuendesha uchaguzi huru na haki nchini.
But What Do I Think I Know?