John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Julai 17, 2021 Rais wa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), Patrice Motsepe alithibitisha kuwa mipango ya kuanzishwa kwa African Super League ipo kwenye hatua nzuri, japo hadi sasa haijawekwa wazi lini hasa michuano hiyo maalum itaanza.
Tetesi ni kuwa huu ndiyo mpunga ambao unatarajiwa kupatikana katika ligi hiyo ambayo uwekezaji wake kwa jumla unatarajiwa kutumia dola milioni 200 (zaidi ya Sh bilioni 461 za Kitanzania):
• Timu 24 zitakazoshiriki CAF Super League zitapewa USD 1m (Sh bilioni 2.3) kama fedha ya wao kushiriki katika michuano hiyo.
• Bingwa atapata USD 10m (Sh bilioni 23)
• Viwanja vyote vitakavyotumika ni vya kiwango cha juu
• VAR itahusika katika kila mechi
• Bingwa wataiwakilisha Afrika katika FIFA Club World Cup
Hii ni fursa kwa klabu za Tanzania zikiwemo Simba, Yanga, Azam FC kupambana kufanikisha kushiriki katika michuano hiyo.