Simba yapoteza kwa Asec Mimosa, lakini kuna fundisho kwa wasio na uzoefu

Ninachokiona Simba inaimarika Sana kwenye game za kimataifa, licha ya kufungwa away lakini performance kujimla ya timu ni nzuri tofauti na miaka ya nyuma.
 
USGM hawajatufunga, tudraw 1-1, update Livescore yako
 
Jana nimeangalia mechi kwa makini Sana.

Kocha abebeshwe lawama.
Pamoja na beki yote ya Simba ikiongozwa na onyango.

Asec wapo mbele bao 3 lakini bado kocha anaingiza washambuliaji.

Simba timu ipo nyuma bao tatu,,
--Badala ya kuingiza attackers matokeo yake unamtoa inonga baka na kuingiza beki ,
Huu ni uchizi.

Kagere peke yake alikuwa hatoshi kuwa threat kwa asec memosa.
Ambayo ilikuwa ikijilinda zaidi na kufanya mashambulizi ya kushtukiza.

Alipaswa aingize striker mwingine acheze na kagere pale mbele.

Onyango --ni mzito Sana,,haendani na Kasi ya Simba kwa sasa ktk mashindano ya kimataifa.

Magoli yote ni uzembe wa mabeki.

Sent from my M2101K7BG using JamiiForums mobile app
 
Hivi kama Simba akishinda dar 6-1 Asec akisuluhu na Berkane inakuaje MNYAMA si anapita enhee ???nipe jibu faster Kuna mtu kaniuliza hapa???
Simba anahitaji ushindi wowote, hata 1-0, wala haitaji mabao mengi. Akishinda wala hakuna haja ya kuangalia matokeo ya mechi nyingine
 
Asec wapo mbele bao 3 lakini bado kocha anaingiza washambuliaji.
Simba timu ipo nyuma bao tatu,,
--Badala ya kuingiza attackers matokeo yake unamtoa inonga baka na kuingiza beki ,
Tatizo ni pale kila mtu anapotaka kuwa mchambuzi. Sijajua uchambuzi wako hapo unamaanisha nini. Kwani attackers si ndio washambuliaji? Labda nitaelewa baadaye
 
Tatizo ni pale kila mtu anapotaka kuwa mchambuzi. Sijajua uchambuzi wako hapo unamaanisha nini
Hsta mimi sijaelewa nini anatamani kusema. Ila mimi kitendo cha kumtoa Inonga na kumuingiza Wawa kimenishangaza sikuelewa kocha alikuwa amefikiria nini kimbinu na kiufundi.
 
Hsta mimi sijaelewa nini anatamani kusema. Ila mimi kitendo cha kumtoa Inonga na kumuingiza Wawa kimenishangaza sikuelewa kocha alikuwa amefikiria nini kimbinu na kiufundi.
Muda wa kufanya sacrifice, unajilipua kukosa kitu fulani kwa ajili ya kutafuta kitu kingine kwa njia ya mkato. inonga yupo bora zaidi kukaba kuliko Wawa. Lakini pia Wawa ana uwezo wa kupiga pasi ndefu kwa usahihi zaidi kuliko Inonga. Kwa muda ule, kocha alihitaji mipira iende mirefu mirefu ikadondokee washambuliaji katika au karibu na eneo la hatari la ASEC, na kazi hiyo akapewa Wawa na alifanya kama mara mbili hivi
 
Umeeleza kwa ufasaha
 
Bora wewe unaetunza kauli kuliko wenzako wenye matokeo mfukoni wanaokwambia kwa Mkapa Hatoki mtu sasa sijui ile match ya Jwaneng ilichezwa Mkwakwani.

Simba imefungwa kwa mkapa baada ya miaka mitano kupita tena mechi moja ni kumaanisha ni nadra sana kufungwa nyumbani kama ilivyo kwa kwa mabigwa wa África pale Egypt [emoji1093] japo walifungwa na mamelodi lakini huwa ni nadra sana
 
Simba akishinda 1-0
Anapita

Ila tukishinda magoli mengi zaidi itapendeza zaidi kama Asec akifungwa goli moja bila na sisi tukashinda goli 3 bila tunaweza kuongeza kundi ili tucheze na timu nafuu kidogo robo fainali
 
relax dada!!kunywa fanta kdg hapoo mtani
 
Ila tukishinda magoli mengi zaidi itapendeza zaidi kama Asec akifungwa goli moja bila na sisi tukashinda goli 3 bila tunaweza kuongeza kundi ili tucheze na timu nafuu kidogo robo fainali
Hakuna namna yoyote kwa sasa itakayoifanya Simba kuongoza kundi. Tie break katika kanuni za mashindano haya zinaeleza kwamba timu zikilingana points, kinachofuata kuangaliwa ni head to head points, then head to head goal difference na kuendelea. Katika head to head points, tumelingana na ASEC na Berkane, ila head to head goal difference, hao wawili wameizidi simba goli moja kila mmoja. Watu wengi hudhani kanuni za mashindano yote duniani zinafanana! No
Kwa hiyo Simba apambane ashinde, moja kwa moja atakuwa namba mbili, na mmoja wao kati ya ASEC na Berkane kwa matokeo yao yoyote atakuwa kinara wa kundi
 
Siku timu za Tanzania sikianza kuwa na uhakika wa matokeo chanya Ugenini ndipo soka letu tutasema limekua, hizi figisu hazisaidii, tujenge timu, tuachane na hizi zimamoto, uchawi, nk
 
Hebu weka hapa goal difference ya mechi 2 za yanga kwenye shirikisho na mechi 5 za Simba shirikisho ndio tuamue nani amebugizwa vya kutosha?
Ushujaa wakati mebugizwa huko vyakutosha.. nyie ni wakufungwa tu miaka yote...
Makoloooooo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…