Simba yasaini mkataba wa Tsh. bilioni 20 na Betway kama Mdhamini Mkuu kwa miaka 3

Simba yasaini mkataba wa Tsh. bilioni 20 na Betway kama Mdhamini Mkuu kwa miaka 3

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Klabu ya Simba ana Jambo kubwa zaidi kuwahi kutokea Afrika, leo Wanasaini dili na mdhamini Mkuu BetWay baada ya M-Bet kusitisha Mkataba wake.

Wakati huo huo wametangaza kuwa Kikosi chao kitaondoka kesho Jumatano kuelekea Ismailia, Misri kwa ajili ya maadalizi ya msimu ujao wa 2025/26.

1753772561488.png
Kaa Karibu hapa kujua mengi ziadi......



Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Simba SC, Zubeda Sakuru, ametangaza udhamini mpya wa Bilioni 20 kutoka Kampuni ya Betway kwa kipindi cha miaka mitatu.

Klabu ya Simba SC imeingia rasmi mkataba huu unaomfanya Betway kuwa mdhamini mkuu wa klabu hiyo kwa miaka mitatu.

Udhamini huo mpya unakuja baada ya Simba kuachana na aliyekuwa mdhamini wake mkuu, kampuni ya M-Bet ambapo mwaka 2023, waliingia mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya TZS Bilioni 26.1.

Simba SC ilikubali ombi la M-Bet la kusitisha nao mkataba.

Screenshot 2025-07-29 104726.png
Zubeda Sakuru - Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Simba SC

"Mkataba ambao tumeingia unakwenda kuleta mapinduzi kwenye mchezo wa soka hapa Tanzania na unakwenda kuongezea nguvu dhamira ya Simba kuwa klabu namba moja barani Afrika."

"Udhamini huu ambao thamani yake ni Bilioni 20 kwa miaka mitatu, unaonyesha namna Simba imedhamiria kuleta mabadiliko ya kuwa klabu kubwa."

1753776175297.png

Salim Abdallah - Mjumbe wa Bodi Simba SC

"Kazi yetu ni kuhakikisha brand yetu ya Simba SC inazidi kukua siku hadi siku, mpira una gharama nyingi timu inahitaji fedha, mashabiki wetu tuwaunge mkono Betway ambao ni wadhamini wetu."

Jimmy Masaoe - Meneja Uendeshaji wa BetWay Tanzania

"BetWay ni kampuni ya kimataifa na yenye uwezo wa kupokea watu wapya hata wakiwa wengi lakini pia tuna huduma kwa wateja ambayo ipo muda wote kuwahudumia."

"Mashabiki wategemee huduma bora kutoka kwetu, tumejipanga. Lakini pia kutakuwa na huduma mbalimbali ambazo tumezibuni kwa ajili ya mashabiki wa Simba."

Jason Shield - Mkuu wa Udhamini wa BetWay Afrika

"Tumeingia Simba sababu ni timu kubwa Afrika, ni timu ambayo inajulikana pande zote za bara hili na hilo ndio tunaangalia zaidi kwenye biashara. Tulikuwa tukiifatilia kwa miaka karibu sita lakini sasa imekuwa kweli. Tunafuraha kufanikisha jambo hili."

"Huu ni zaidi ya ushirikiano na inatakiwa klabu zote zifaidike na jambo hili. Tunashirikiana na timu nyingi kubwa ambazo tunadhamini hivyo uzoefu huo utatusaidia kufanikisha jambo hili."

"Nina furaha kwa ushirikiano huu lakini tutafanya kazi kuangalia namna gani ya kufanikisha ushirikiano na vilabu vingine vikubwa ambavyo tunashirikiana navyo."

1753777004438.png


Athuman Nyamlani, Makamu wa Kwanza wa Rais TFF - Mwakilishi wa mgeni rasmi

"Nitoe pongezi kwa Simba, ni tukio ambalo kila siku TFF tunaliimba, ni hatua kubwa. Sisi TFF tunasisitiza kila upande uhakikishe unatimiza wajibu wake. Lakini mafanikio haya ya kupata udhamini mkubwa yanatokana na ubora wa ligi yetu sababu inaendelea kuimarika kila siku. Wito wetu sisi ni uwazi kwenye matumizi ya pesa zinazotolewa na wadhamini maana utatusaidia kuaminika na wadhamini."

"Tutumie fedha hizi kuimarisha timu. Mkataba wa Bilioni 20 ni fedha nyingi sana, zitumike vizuri na ikiwezekana siku moja tuitwe tena kusaini mkataba mkubwa zaidi."
 
Betway miaka mitatu bil 20,mo dewji kanunua timu maisha kwa bil 20 hyo hyo na matangazo anafanya kwa bei ya nyanya,Simba bado Sana,mambo yao upande wa mwekezaji yamekaa kimagumashi Sana,siwezi kuvaa hyo jezi taka taka
 
Mbumbumbu fc kazi Yao ni kujitekenya na kucheka wenyewe, Ndani ya hii miaka mitano wame saini mikataba ya mamilioni ya shilingi lakini inaonekana Bado timu Ina struggle katika sajili zake.

Ni jambo la kushangaza timu Ina saini mikataba mikubwa katika makaratasi lakini katika usajili ambao indio Moja ya Asset za klabu Ina boronga vibaya kufikia kuweka (min budget) katika ya msimu kwaajili ya hongo na matokeo ya mchongo.
 
Back
Top Bottom