Simba yasaini mkataba wa Tsh. bilioni 20 na Betway kama Mdhamini Mkuu kwa miaka 3

Simba yasaini mkataba wa Tsh. bilioni 20 na Betway kama Mdhamini Mkuu kwa miaka 3

GSM anajinufaisha na Yanga kujitaangazia biashara zake na haijulikani anaipa kiasi gani yanga
Gsm anaipa ubingwa yanga na mwakani ni mara ya Tano mfululizo hiyo ni zaidi ya pesa shabiki yake furaha ya makombe pesa hazituhusu ni zao sisi hatupati kitu zaidi ya furaha ya makombe mda huo gsm sio mmiliki wa yanga
 
Gsm anaipa ubingwa yanga na mwakani ni mara ya Tano mfululizo hiyo ni zaidi ya pesa shabiki yake furaha ya makombe pesa hazituhusu ni zao sisi hatupati kitu zaidi ya furaha ya makombe mda huo gsm sio mmiliki wa yanga
Hichi ulichoandika ndo akili za kinyumbu zenyewe
 
Hichi ulichoandika ndo akili za kinyumbu zenyewe
We ndio nyumbu hushtuki timu Kila mwaka inaingia mikataba ya mabilioni ila mwaka wa nne huu Haina kombe lolote we kama shabiki hunufaiki na chochote hapo pesa zinawahusu wao viongozi sio wewe mpiga kelele
 
Sasa kama betway Wana Saini mkataba WA bil. 20, jay rutty nae kasaini mikataba WA mabilioni

Sasa hizo Ela anazosema mo Huwa anatumia, Mara Simba inamfilisi.

Atwambie Huwa anazifanyia Nini pale simba?
 
We ndio nyumbu hushtuki timu Kila mwaka inaingia mikataba ya mabilioni ila mwaka wa nne huu Haina kombe lolote we kama shabiki hunufaiki na chochote hapo pesa zinawahusu wao viongozi sio wewe mpiga kelele
Kwa akili hizi huna tofauti ni Chief Mangungo wa msovero
 
Sasa mashabiki wote tunahamia kwa Betway na bilioni 20 yao! Hatujaambiwa mkataba na mwekezaji Mo unaingiza kiasi gani kwa mwaka! Hatujaambiwa mkataba wa bilioni 26+ na Mbet mpaka wanatupa taulo ulingoni uliingizia timu bilioni ngapi kati ya hizo 26+!!

Bado kuna mkataba wa bilioni za kutosha na Jayruty! Sijui na wenyewe umeishia wapo! Halafu wakati huo huo Mwenyekiti Mangungu anatuletea Caesar Manzoki kwenye uchaguzi, na tunampa kura! Ismail Rage na Mwina Kaduguda wanatuita mbumbumbu sisi mashabiki, na bado tunaridhika tu! Mwekezaji kila siku anatangaza kupata hasara, lakini anaendelea tu kukomaa na timu yetu!

Miaka 4 mfululizo hakuna ubingwa, na bado hatuandamani kumuondoa mwenyekiti na watu wake!
 
Klabu ya Simba ana Jambo kubwa zaidi kuwahi kutokea Afrika, leo Wanasaini dili na mdhamini Mkuu BetWay baada ya M-Bet kusitisha Mkataba wake.

Wakati huo huo wametangaza kuwa Kikosi chao kitaondoka kesho Jumatano kuelekea Ismailia, Misri kwa ajili ya maadalizi ya msimu ujao wa 2025/26.

Kaa Karibu hapa kujua mengi ziadi......



Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Simba SC, Zubeda Sakuru, ametangaza udhamini mpya wa Bilioni 20 kutoka Kampuni ya Betway kwa kipindi cha miaka mitatu.

Klabu ya Simba SC imeingia rasmi mkataba huu unaomfanya Betway kuwa mdhamini mkuu wa klabu hiyo kwa miaka mitatu.

Udhamini huo mpya unakuja baada ya Simba kuachana na aliyekuwa mdhamini wake mkuu, kampuni ya M-Bet ambapo mwaka 2023, waliingia mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya TZS Bilioni 26.1.

Simba SC ilikubali ombi la M-Bet la kusitisha nao mkataba.

Zubeda Sakuru - Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Simba SC

"Mkataba ambao tumeingia unakwenda kuleta mapinduzi kwenye mchezo wa soka hapa Tanzania na unakwenda kuongezea nguvu dhamira ya Simba kuwa klabu namba moja barani Afrika."

"Udhamini huu ambao thamani yake ni Bilioni 20 kwa miaka mitatu, unaonyesha namna Simba imedhamiria kuleta mabadiliko ya kuwa klabu kubwa."


Salim Abdallah - Mjumbe wa Bodi Simba SC

"Kazi yetu ni kuhakikisha brand yetu ya Simba SC inazidi kukua siku hadi siku, mpira una gharama nyingi timu inahitaji fedha, mashabiki wetu tuwaunge mkono Betway ambao ni wadhamini wetu."

Jimmy Masaoe - Meneja Uendeshaji wa BetWay Tanzania

"BetWay ni kampuni ya kimataifa na yenye uwezo wa kupokea watu wapya hata wakiwa wengi lakini pia tuna huduma kwa wateja ambayo ipo muda wote kuwahudumia."

"Mashabiki wategemee huduma bora kutoka kwetu, tumejipanga. Lakini pia kutakuwa na huduma mbalimbali ambazo tumezibuni kwa ajili ya mashabiki wa Simba."

Jason Shield - Mkuu wa Udhamini wa BetWay Afrika

"Tumeingia Simba sababu ni timu kubwa Afrika, ni timu ambayo inajulikana pande zote za bara hili na hilo ndio tunaangalia zaidi kwenye biashara. Tulikuwa tukiifatilia kwa miaka karibu sita lakini sasa imekuwa kweli. Tunafuraha kufanikisha jambo hili."

"Huu ni zaidi ya ushirikiano na inatakiwa klabu zote zifaidike na jambo hili. Tunashirikiana na timu nyingi kubwa ambazo tunadhamini hivyo uzoefu huo utatusaidia kufanikisha jambo hili."

"Nina furaha kwa ushirikiano huu lakini tutafanya kazi kuangalia namna gani ya kufanikisha ushirikiano na vilabu vingine vikubwa ambavyo tunashirikiana navyo."



Athuman Nyamlani, Makamu wa Kwanza wa Rais TFF - Mwakilishi wa mgeni rasmi

"Nitoe pongezi kwa Simba, ni tukio ambalo kila siku TFF tunaliimba, ni hatua kubwa. Sisi TFF tunasisitiza kila upande uhakikishe unatimiza wajibu wake. Lakini mafanikio haya ya kupata udhamini mkubwa yanatokana na ubora wa ligi yetu sababu inaendelea kuimarika kila siku. Wito wetu sisi ni uwazi kwenye matumizi ya pesa zinazotolewa na wadhamini maana utatusaidia kuaminika na wadhamini."

"Tutumie fedha hizi kuimarisha timu. Mkataba wa Bilioni 20 ni fedha nyingi sana, zitumike vizuri na ikiwezekana siku moja tuitwe tena kusaini mkataba mkubwa zaidi."

Karibu bilioni 7 Kila mwaka hongereni ila kimbukeni kutakuwa na nyongeza kwenye bilioni 67 kwenye madai
 
Back
Top Bottom