Kutoka kwenye ukurasa wa James Sheka
PA OMAR JOBE ni mshambuliaji kutoka Gambia ambaye amezaliwa mwaka 1998 huko nchini kwao Gambia akicheza katika eneo la ushambuliaji wa kati lakini pia ana uwezo wa kucheza nyuma ya mshambuliaji pia kama winga.
Pa Omar JOBE, wakati anatambulishwa na klabu ya Simba ametokea ligi ya KAZAKHSTAN huko Ulaya Mashariki ambako amecheza michezo 25, akishinda magoli 13 na pasi za magoli yaani assists (5).
So far so good Kwa hizi takwimu hizi bila shaka ni mshambuliaji mzuri Sana, lakini pia amecheza michezo 67 katika vilabu mbalimbali alivyopita alifanikiwa kufunga magoli 39 na pasi za usaidizi wa magoli yaani assists 10 katika ligi tofauti tofauti alizocheza ikiwemo pia ligi ya Bangladesh.
Bila shaka Kwa kumwangalia ni mchezaji mzuri Sana, Movement zake, Touches zake, uwezo wake wa kupiga mashuti, uwezo wake wa kufunga magoli ya vichwa, uwezo wa kupiga pasi pia footwork yake Iko vizuri Sana.
Ni mshambuliaji mwenye nguvu na kasi anapokuwa na mpira ni ngumu Kwa mpinzani kumpokonya mpira anapomiliki mpira, kutokana na umahiri wa viungo wengi wa Simba akiwemo SAIDO NTIBAZONKIZA, LUIS JOSE MIQUISSONE pamoja na Chama bila shaka kama akiweza ku-adapt mazingira ya ligi yetu, utamaduni wa Tanzania na akiweza kuwa na mahusiano mazuri na wenzake naamini atafanya vizuri Sana.
Cha msingi wapenda soka lakini pia wasimba na mashabiki wao, wamvumilie tu maana hapa Tanzania Kuna mambo mengi Sana, mchezaji anaweza akaja ana kiwango kizuri tu lakini akaja akashindwa kufanya vizuri.
Wachezaji wanatofautiana Sana katika kuzoea mazingira Kwa uharaka, wengine Wana uwezo wa kuzoea haraka lakini wengine Wanazoea pole pole, na Kuna mchezaji anaenda timu fulani akiwa na kiwango lakini baada ya kufika akashindwa kufanya vizuri.
Kuna mifano mingi Sana, akiwemo Angel Di Maria kutoka Real Madrid kwenda Manchester united FC lakini hakufanya vizuri, Radamel Falcao kutoka Monaco FC kwenda Manchester united FC hakufanya vizuri, Memphis Depay kutoka PSV FC kwenda Manchester united FC hakufanya vizuri, James Rodriguez kutoka Monaco FC kwenda REAL MADRID hakufanya vizuri.
@officialmohamedi_tz
@jamessheka78
#HOLYFINGERS was here.