Simba yashikwa sharubu bila kufurukuta na African Lyon, yalala kwa goli moja Uhuru Nov 6, 2016

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001


Simba Sc timu iliyocheza mechi 13 na kufungwa goli 2 tu na moja la mkono ililofungwa na Yanga SC,leo inakipiga na African Lyon ya Dar es Salaam uwanja wa Uhuru. Mechi hiyo itakuwa ni ya 14 kwa Simba-Taifa Kubwa ikiwa imeiacha mpinzani wake Yanga (aliyefungwa na Mbeya City na Stand Utd) kwa pointi 8, imejikusanyia jumla ya pointi 35

Mechi hiyo itapigwa jioni saa 10 na itarushwa live na Azam TV na kutangazwa na TBC one na Uhuru FM. Hapa JF nitakuletea moja kwa moja mtanange huu kwa msaada wa Azam TV

Simba inategemewa kuendeleza kipigo kwa kila timu inayokutana nayo bila kujali wepesi au uzito wake.
Hivi punde ntakuletea kikosi kizima cha Mnyama Taifa Kubwa
Usiondoke

Updates....................................
KIKOSI CHA SIMBA SC-TAIFA KUBWA
1. Vicent Angban
2. Javier Bukungu
3. Mohamed Zimbwe
4. Novart Lufunga
5. Method Mwanjale
6. Jonas Mkude
7. Muzamiru Yassin
8. Mwinyi Kazimoto
9. Laudit Mavugo
10. Mohamed Ibrahim
11. Shiza Kichuya

AKIBA:
1. Peter Manyika
2. Hamad Juma
3. Said Ndemla
4. Moussa Ndusha
5. Emmanuel Semwanza
6. Jamal Mnyate

=========
Matokeo ya Mechi zote za VPL Leo.
 
Mnyama tafuna afrika huyo akabebe makopo mbagala
 
Ni Simba vs African Lyon ( sio Leon).

Mungu ibariki Simba Sc.

[HASHTAG]#UmojaNiUshindi[/HASHTAG]
 
Kwani walicheza jana? Leo tar 6 mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…