Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
"Zile zama za kuwa na mkataba sare sare maua zimepita. Kwa miaka ya hivi karibuni Simba tumewekeza vya kutosha ili kuhakikisha brand yetu inakua,"- Meneja wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally.
“Process ya mdhamini mpya tulianza tangu mwaka jana. Tumepokea boss nyingi za kutaka kuwa main sponsor, lakini M-Bet ndio wamekidhi vigezo vyetu vyote,” - CEO wa Simba, Barbara Gonzalez.
"Kwa ukubwa wa Simba ni lazima kujihusisha na kampuni ambayo inaongoza kwenye biashara ambayo wanafanya. Mkiangalia takwimu M-Bet wanaongoza kwa ukubwa Tanzania."- Barbara
"Hii ni mara ya kwanza mdhamini mkubwa anakuwa na senior team pekee, huko nyuma mdhamini mkuu alikuwa kwa timu zote lakini sasa timu zingine tunaweza kuzitafutia mdhamini wake,"- CEO
Mkurugenzi wa Masoko wa M-Bet, Allen Mushi ametaja mchanganuo wa udhamini mpya wa Klabu ya Simba:
Mwaka wa kwanza - Bil 4.670
Mwaka wa pili - Bil 4.925
Mwaka wa tatu - Bil 5.205
Mwaka wa nne - Bil 5.514
Mwaka wa tano - Bil 5.853
Jumla ni Bilioni 26, Milioni 168 na Tsh. 5,000.
=================================
TUJIKUMBUSHE MKATABA WA YANGA
Yanga SC ilisaini mkataba mpya wa Udhamini Mkuu na Kampuni ya kubashiri ya Sportpesa Tanzania, wenye thamani ya Tsh 12.3B kwa miaka mitatu (3), ambayo ni sawa na 4.1B kwa kila mwaka.
Mkataba huo ni ongezeko la Tsh bilioni 2 kwa mwaka kutoka kwenye mkataba awali wa bilioni moja kwa mwaka mmoja.
Pia soma:
Yanga FC yaingia mkataba mpya na SportsPesa wa miaka 3 wenye thamani ya Tsh Bilioni 12