Simba yaweka rekodi ya timu za Bara kwa kupiga pasi 873

Lupweko

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2009
Posts
23,566
Reaction score
24,891
Katika mechi ya Simba vs Dodoma Jiji, timu ya Simba ilipiga jumla ya pasi 873 na kati ya hizo, pasi 730 zilifika zilikopangwa kwenda. Takwimu hizi ni kwa mujibu wa Anwar Binda wa Wasafi FM wakati akichambua mechi hiyo, na kusema tangu aanze kuchambua mechi za VPL na ASFC za timu za Tanzania Bara, hakumbuki kama kuna timu imewahi kupiga idadi kubwa ya pasi kama hizo.

Hongera wazee wa Lunyasi kwa kuleta mapinduzi ya burudani katika soka hapa Bongo.
 
Huu ndio upuuzi tunao jivunia nao, mpaka ukija kuamka na kugundua kua Mataji ni muhimu kuliko pasi...wenzetu watakuwa mbali sana.
 
Subiri wakuje wale walima mchicha mashuhuri waje kukusulubu na Greenwich yao.
 
Kwa tafsiri nyingine ni kwamba Simba nayo ni Bingwa wa kihistoria wa kupiga pasi nyingi hapa Tanzania Bara..
 
Hakuna bingwa wa kihistoria, ila kupiga pasi ni moja ya mbinu za kumiliki mpira. Fikiria mtu yupo nyuma kwa bao 2-0 halafu anahaha kuutafuta mpira ulipo, hayo ni mateso makubwa Simba inayatoa, na matokeo yake anayetafuta mpira anajikuta anapigwa lingine
 
Katika mechi ya Simba vs Dodoma Jiji, timu ya Simba ilipiga jumla ya pasi 873 na kati ya hizo, pasi 730 zilifika zilikopangwa kwenda. Takwimu hizi ni kwa mujibu wa Anwar Binda wa Wasafi FM wakati akichambua mechi hiyo, na kusema tangu aanze kuchambua mechi za VPL na ASFC za timu za Tanzania Bara, hakumbuki kama kuna timu imewahi kupiga idadi kubwa ya pasi kama hizo.

Hongera wazee wa Lunyasi kwa kuleta mapinduzi ya burudani katika
 
Hakuna bingwa wa kihistoria, ila kupiga pasi ni moja ya mbinu za kumiliki mpira. Fikiria mtu yupo nyuma kwa bao 2-0 halafu anahaha kuutafuta mpira ulipo, hayo ni mateso makubwa Simba inayatoa, na matokeo yake anayetafuta mpira anajikuta anapigwa lingine
Hiyo ilitokana na yale majimaji yaliyomwagwa vyumbani. Yale maji yalitumika pia kwenye game ya Kaiza.
Ndio maana Yanga machale yaliwacheza mapema tu.
 
Sawa wazee wa kupindua meza
20210523_073951.jpg
 
Sawa wazee wa tumetolewa kwa mbinde, na kubakwa itakua kwa mbinde pia
 
Daah! Nimekumbuka chelsea walikuwa wanamsufia jojinho kwa kupiga mipasi ilifikia hatua kwa game anapiga pasi hadi 200 pekeyake, balaa likaja timu inafanya hovyo na jamaa hana assist hata moja ndio wakastuka pasi nyingi haziwasaidii chochote
 
Huu ndio upuuzi tunao jivunia nao, mpaka ukija kuamka na kugundua kua Mataji ni muhimu kuliko pasi...wenzetu watakuwa mbali sana.
Mataji gani tena..Hayo mataji muhimu kwa Simba tu, Yanga mwaka wa ngapi hajui VPL wala ASFC

Kwa Simba ni falsafa yake, pasi milioni, haikwepeki kama Barcelona huwezi kuwalazimisha wabutue.
 
Back
Top Bottom