Simbachawene hizi rushwa za polisi zinatuumiza sisi wapenda usingizi, baa zisizo na vibali zashamili Tegeta, Boko, Bunju

Simbachawene hizi rushwa za polisi zinatuumiza sisi wapenda usingizi, baa zisizo na vibali zashamili Tegeta, Boko, Bunju

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
13,778
Reaction score
7,145
Wana Jf

Nawatoe wasiwasi wapenda raha , lakini kila mtu ana raha yake kutokana na mazingira inayoishia. Wapo wanaooenda kukesha kama popo na milupo pembeni, lakini wapo pia baada ya kupata tatu na nne bariidi wanapenda wakapunzike na mama chanja.

Kumekuwepo na utitiri wa baa zisizo na vibari vya kukesha linapita mziki mkubwa vikichochewa na Ma DJ usiku unasikia "Wananchi piga keleeeleee" nao wakaitikia "Bia Tamuuuu" inapendeza kujiunga nao lakini wengine hatupendi muda wa mapopo, si ijumaa wala jmamosi watu wanakesha baa za wazi, ikifika saa sita utaona cruiser siku hizi hakuna defender, watashuka kwenye gari za kitalii, utaona meneja anatoka nao mita kadhaa anazama mfukoni kuwezesha mafuta ya cruiser lisirudi bure.

Watz tunapenda raha lakini tusiumize wengine, mbona makanisa yakilokole yaliyokuwa yanakesha wameacha makelele kwa sasa. Hivi sasa wamebaki wanaosumbua asubuhi na maspika yao ni wa zile dini zisizoguswa hata zifanye mini.

Angalau wao wanaanza saa kumi unakuwa ushakata usingizi wa kwanza. Polisi jamani kuweni na huruma, hizi rushwa zinaumiza wapenda usingizi Tegeta, Boko, Bunju.
 
Washaurini wamiliki wa night clubs waweke sound proof....
 
Ila kweli , nishaishuhudia najua wana kumbe watu wa kazi
Kuna kijiwe juzi usiku masela wamebebwa kindezi,

Police walikuja na gari imebandikwa maua Fulani Kama inaenda harusini,mara wazee gafla wakawarukia masela tembeza Sana virungu ,wameondokanao Kama nane hivi, nimeambiwa Bado wapo Central police
 
Unataka tule wapi kaa kwa kutulia dawa iwangie kwanza maslahi yetu duni na makazi sio salama

Kila mtu atakula kwa urefu wa kamba so acha umbea
 
Police Tanzakiza
JamiiForums-289452902.jpg
 
Wana Jf

Nawatoe wasiwasi wapenda raha , lakini kila mtu ana raha yake kutokana na mazingira inayoishia. Wapo wanaooenda kukesha kama popo na milupo pembeni, lakini wapo pia baada ya kupata tatu na nne bariidi wanapenda wakapunzike na mama chanja...
Siwapendi polisi kabisa. Ila kama wanachukua rushwa ili tuendelee kupiga ulabu... kwa mara ya kwanza niko upande wao. Wachukue rushwa za kutosha wanywaji tupige gambe mama Samia apate hela za kutosha kusomesha na kutibu watoto wetu

Akikwambie mtu K Vant ni tamu kuliko bia... tena ni tiba ya CORONA. Ukiipiga na Kitimoto, virusi vya ukimwi vinadedi...
 
Vibali hawatoi polisi ni Afisa Biashara wa Halamshauri ndiye anatoa vibali vya bar kukesha au sherehe
 
Wana Jf

Nawatoe wasiwasi wapenda raha , lakini kila mtu ana raha yake kutokana na mazingira inayoishia. Wapo wanaooenda kukesha kama popo na milupo pembeni, lakini wapo pia baada ya kupata tatu na nne bariidi wanapenda wakapunzike na mama chanja...
Chalamaila anasema Acga watu wale Bia
 
Siwapendi polisi kabisa. Ila kama wanachukua rushwa ili tuendelee kupiga ulabu... kwa mara ya kwanza niko upande wao. Wachukue rushwa za kutosha wanywaji tupige gambe mama Samia apate hela za kutosha kusomesha na kutibu watoto wetu

Akikwambie mtu K Vant ni tamu kuliko bia... tena ni tiba ya CORONA. Ukiipiga na Kitimoto, virusi vya ukimwi vinadedi...
Nami mpendwa raha lakini madha wanazidisha utasikia "tender Twendeee pigs keleleleeee" Bia taaamu , tatizo maspikanmakubwa kama ya Gwajima akipiga kelele, mama ni kwa sauti ya chini hakuna shida kabisa yaani
 
Back
Top Bottom