Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema katika operesheni ya kuwasaka majambazi inayoendelea nchini kati ya majambazi kumi wanaokamatwa mitaani, watatu wanatoka gerezeni.
Amesema kuwafunga majambazi hao hakusaidii sana kwa sababu wanarudi mitaani na kuendelea kufanya uhalifu wa aina mbalimbali pamoja na kuwaua watu wenye haki, hivyo watatafuta namna nyingine ambayo watamalizana na majambazi hayo.
Waziri Simbachawene amezungumza hayo katika Kata ya Pwaga, Jimbo la Kibakwe, Wilayani Mpwapwa, katika ziara yake inayoendelea ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni kwake, ambapo amesema licha ya kuwa wamemalizana na majambazi hayo lakini bado Jeshi la Polisi linaendelea na operesheni ya kuwasaka itakayo kamilika Julai 28, mwaka huu.
Aidha, Waziri Simbachawene alisema wanaohusika na uhalifu ni watu wanaotoka katika jamii, wananchi wanawajua, ili kudhibiti matukio ya uhalifu wananchi hao wanapaswa kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kuwafichua wanaofanya uhalifu huo katika sehemu wanazoishi.
Alisema Jeshi la Polisi haliwezi kuwa na askari kila mahali ni jukumu la wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa ajili ya usalama wao kwa kutoa taarifa sahihi juu ya uhalifu na wahalifu, lakini pia kwa kushiriki katika ulinzi pamoja na Jeshi la Polisi na ndiyo tunaita ulinzi shirikishi.
PIA SOMA:
- Waziri Simbachawene: Majambazi yamenyamazishwa kimyakimya nchini, msako wabakaji, waporaji waendelea