Simbachawene: Kati ya majambazi 10 wanaokamatwa, 3 wanatoka gerezani

Simbachawene: Kati ya majambazi 10 wanaokamatwa, 3 wanatoka gerezani

Asiiishie kumalizana na majambazi tu bali kama waziri ana jukumu la kumshauri Rais kubadili huu mfumo wa kuwasamehe wafungwa. Ikiwezekana Wezi na majambazi wasiwe sehemu ya wanaopata msamaha huo.
 
Kule Kenya walianzisha ATPU mwaka 2003 Kwa ajili ya "magaidi".

Wanamalizana na suspects "Juu Kwa juu" yaani hata walioshinda kesi mahakamani wakiingia uraiani wanawindwa,wanakula shaba.

Masheikh wa Mombasa hasa Masjid Musa ni mfano wa wahanga wa ATPU.
 
Pertinent observation! Yaani asilimia 70% ya majambazi hawajawahi kufungwa gerezani. Haya juhudi za kuwakamata na kuwafunga ziendelee.
Hakuna cha petinti wala nini. Haya ni mambo ya uwiano. Chukulia watanzania waliowahi kufungwa huko jela ni asilimia sifuri nukta moja, yaani moja kwa elfu moja, lakini linapokuja suala la wanaokamatwa kwa ujambazi kibso kinageuka. Kwa kila majambazi mia wanaokamatwa, 30 walishawahi kufungwa jela, yaani hesabu imetoka moja kwa elfu moja hadi thelasini kwa mia. Hapo lazima kuna tatizo kubwa sana. Mh. Waziri hajakosea.
 
0.1 ni sawa na 1/1000? Labda ndiyo maana huoni kosa la waziri wako.
 
Ni kati ya viumbe hatari sana, hawana huruma...
 
Back
Top Bottom