Simbachawene kemea maovu na uvunjifu wa haki za binadamu unaofanywa na polisi

Simbachawene kemea maovu na uvunjifu wa haki za binadamu unaofanywa na polisi

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Kila siku imayoenda kwa Mungu tunasakikia malalamiko ya wananchi juu ya askari polisi kufanya vitendo vya kikatili dhidi ya raia. Lakini waziri mwenye dhamana yupo kimya tu hatoi tamko wala kukemea.

Mfano ni huko Handeni tumeshuhudia akina mama wakilalama hadharani kupigwa na kutomaswa kwa nguvu na askari polisi lakini Waziri amekuwa kimya tu.

Majuzi tu huko Dodoma polisi wanadaiwa kumkamata kijana dereva wa boda boda na kumpiga na kisha kumuingizia mti kwenyd njia ya haja kubwa na nusura afariki . Lakini mpaka sasa Simbachawene Waziri yupo quite.

Hakuna anayetetea mharifu anayekuwa na siraha na kutaka kupambana na polisi kisha akauwawa. Lakini vipi hawa wanaokamatwa na kutii kisha kupigwa na kuteswa? Mbona waziri hakemei kitu?

Vipi kuhusu wanaopigwa na kuteswa kisa tu wanatuhumiwa bila kufikishwa mahakani? Mbona Simbachawene hakemei?
 
hivi ndio vyazo vya watu wanafikia hata kujitoa muhanga tu poa.uondoke hata na wawili wa3.
 
Serikali ya CCM haina uchungu na wananchi kwasababu imeingia madarakani kwa wizi wa kura.
 
Back
Top Bottom