Simbachawene: Kushusha kiwango cha Faini kwa Bodaboda haina Maana wavunje Sheria. Asema kimya Kimetawala kwenye ujambazi

Simbachawene: Kushusha kiwango cha Faini kwa Bodaboda haina Maana wavunje Sheria. Asema kimya Kimetawala kwenye ujambazi

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Waziri wa Mambo ya Ndani, Simbachawene akiongea mbele ya Rais Samia amesema pamoja na uamuzi mzuri wa kushusha kiwango cha faini kwa Bodaboda haina maana kwa vijana kwa vijana watumie nafasi hiyo kuvunja sheria ya usalama barabarani.

Simbachawene amesema pamoja na jitihada zinazofanywa na Jeshi la Polisi bado vijana wengi wanapotea kwa Vifo akitolea mfano mwaka 2020, ajali za bodaboda na bajaji zilikuwa 404 na kusababisha vifo 281 na kuacha majeruhi 320.

Amesema vifo na ulemavu vinatia umasikini familia na vijana ndio wanaotegemewa na wazazi na watoto wao.

Kuhusu Ujambazi, Simbachawene amesema kuna watu waliwabip na wao wameamua kuwapigia na kwasasa kimya kimetawala na kwa sasa wanaendelea na operesheni nchi nzima.


 
Waziri wa Mambo ya Ndani, Simbachawene akiongea mbele ya Rais Samia amesema pamoja na uamuzi mzuri wa kushusha kiwango cha faini kwa Bodaboda haina maana kwa vijana kwa vijana watumie nafasi hiyo kuvunja sheria ya usalama barabarani...
Uhitaji kuwa na Degree kulijua hilo Adhabu kubwa japo haufanyiki Makosa hayatendeki lakini inapunguza Makosa kwani inaogopesha
Lakini Adhabu ndogo inaongeza Makosa kwani Haitishi na mkosaji anaweza kuilipa
 
Back
Top Bottom