Simbachawene: Serikali kuangalia upya utaratibu wa kuanzisha Makanisa, Wachungaji watapaswa kuwa na Shahada ili kupunguza "Vibanda Imani"

Si kila kitu cha kuiga kutoka Rwanda , mmeiga utekaji inatosha mengine jiongezeni , wekeni tu utaratibu mzuri wa kudhibiti umati basi , Yesu Kristo alikuwa na digrii ngapi ?

Wame sahau kwamba mwanzo Yesu Kristo alikuwa fundi seremala!!
 
Safi sana. Bila kuwasahau mashekh. Bila shahada hakuna kuswalisha msikitini. Watu wanauziwa mafuta ovyo ovyo kisa upako. Mtu mwenye shahada hawezi kubeba fimbo kuchapa watu kisa hajafunga au wanapika hadharani siku ya ramadhani.
Mshenga Gwajima ana PhD
Lusekelo itabidi akaitafute shahada,
 
Mchungaji awe na shahada lakini mbunge ajue kusoma na kuandika tu...hakika kuna sehemu tunakosea tena pakubwa sana
 
Bila kuwasahau mashekh. Bila shahada hakuna kuswalisha msikitini. Watu wanauziwa mafuta ovyo ovyo kisa upako. Mtu mwenye shahada hawezi kubeba fimbo kuchapa watu kisa hajafunga au wanapika hadharani siku ya ramadhani.
Wame sahau kwamba mwanzo Yesu Kristo alikuwa fundi seremala!!
 
Na yesu alilisha watu elfu 5 mikate na samaki wakala na kushiba lkn siku hizi watu elfu 5 wanamlisha nabii 1 ili aendeshe helikopta,alipie walinzi wake,aendeshe magari ya kifahari.
Wame sahau kwamba mwanzo Yesu Kristo alikuwa fundi seremala!!

dodge
 
Ni fursa sasa kwa taasisi za elimu ya juu kuanzisha shahada ya Teolojia kwenye vyuo vyao.
 
Mshenga Gwajima ana PhD
Lusekelo itabidi akaitafute shahada,
Mbona hata gwajiboi mzee phd wakati anatoka alisema anafufua wafu na hapo ndipo alipoliweza gemu.. Kwahiyo uongo hauangalii phd wala diploma ni mradi nitoke vp.
 
Leo unawaita vibanda Imani siyo! kwa ajili ya uwaziri wa mabo ya ndani?

Na waganga wote wa jadi wawe na shahada. maana na wao ni vibanda imani.
 
Akili za wanaccm wanazijua wenyewe. Hapo wameangalia upande mmoja tu. Je kuhusu mashekh? Ndiyo yale ya utumbuaje wa vyeti feki halafu JWTZ haiguswi na idara zingine. Hapo inakuwa siyo sheria ni ukandamizaji.
Mchungaji awe na shahada lakini mbunge ajue kusoma na kuandika tu...hakika kuna sehemu tunakosea tena pakubwa sana
 
Then waweke masharti ili kanisa lako lisajiliwe lazima uwe na jengo la kudumu(sio haya maturubai yanayotumika),uwe na vizuia sauti ndani ya jengo(sound proof),uwe na uwezo wa ku-rescue waumini incase of emergency na degree ya theology juu.

Tutakua tumepata mahala pazuri pa kuanzia.
Ni fursa sasa kwa taasisi za elimu ya juu kuanzisha shahada ya Teolojia kwenye vyuo vyao.

dodge
 
Ni fursa sasa kwa taasisi za elimu ya juu kuanzisha shahada ya Teolojia kwenye vyuo vyao.
atasoma nani akafanye kazi wapi.Makanisa vijijini hayana watu wala sadaka
hata haya makubwa YA DINI KUBWA unayoayaona yamefikia saturation point hayahitaji

Hao unaowaona wanaanzisha ni karama zao tu ndizo zinawasaidia

kuna kitu waziri haelewi kuwa wasisoma wana makanisa yao wakiongozwa na wasiosoma wenzao
matabaka hayaepukiki kwenye jamii kuna mmisikiti na makanisa kwa ajli ya elites watu wa juu wasomi nk na kuna hao akina hohe hahe wasio na nafasi kwenye makanisa makubwa kwa sababu za kubaguliwa kielimu au kimapato au social status.Hao hawahitaji na hawataki wenye digrii wanataka wenye karama na vipawa tu

ukiweka misharti ya midgrii utatengeneza wapagani wengi wasiosali popote na ni hatari kwa usalama wa nchi sababu hawako tayari kuongozwa na digrii hawataenda sali popote.

hao watu ni lowest class wengi kwenye society umakini unatakiwa kufikia maamuzi na uhusishe idara zote nyeti zikiongozwa na usalama wa taifa.HILI Si la mtu mmoja au wawili tu kuamua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…