Simbachawene: Serikali kuangalia upya utaratibu wa kuanzisha Makanisa, Wachungaji watapaswa kuwa na Shahada ili kupunguza "Vibanda Imani"

Simbachawene: Serikali kuangalia upya utaratibu wa kuanzisha Makanisa, Wachungaji watapaswa kuwa na Shahada ili kupunguza "Vibanda Imani"

Naona Waziri anaongea mambo yasiyohusiana. Ajali ilisababishwa na Wahubiri kutokuwa na Shahada? Wahubiri wengi mbona wana shahada? Je tatizo ni Sera? Sheria?
Tatizo kubwa linaweza kuwa Sheria,Kanuni na Taratibu kufuatwa kwa ukamilifu.. Pia kulikuwa na Menejimenti mbovu ya eneo la Mkusanyiko..
Watu wa kulaumu wa kwanza ni walinda Usalama yaani Polisi. Wao walitoa kibali? Walikisimamia hadi mwisho?
Kwa hiyo Waziri wa Mambo ya Ndani anagushwa moja kwa moja.. kitu alichokuwa akikikwepa Waziri..
Kuhusu Sheria,Kanuni na Taratibu inabidi ziboreshwe ili kuendana na wakati.
  • Watu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wahusishwe katika ukaguzi wakati wa kufanya maandalizi ya eneo la mikusanyiko ya halaiki.
  • Magari ya Wagonjwa yawepo kwa gharama za waandaji wa mikutano ya halaiki.
  • Magari ya Uokozi angalau ya Binafsi.
  • Polisi wasimamie vibali vyao.
  • Waandaaji watumie busara na weledi kidogo.
 
Waziri wa mambo ya ndani Mh Simbachawene amesema kufuatia vifo vya watu 20 kwenye Huduma ya Mwamposya huko Moshi, serikali itaangalia upya utaratibu wa kusajili hizi Huduma.

Simbachawene amesema Wachungaji wanaoanzisha Huduma za kiimani watapaswa kuwa na shahada ili kupunguza " Vibanda Imani" vilivyozagaa kila kona.

Rwanda wamefanikiwa kudhibiti Vibanda Imani kwa kutumia utaratibu huu, amesisitiza Simbachawene.

Source Clouds tv!
Kwani tatizo ni aina ya mafunndisho au ni taratibu za kiusalama zilizopelekea vifo? Kwani kuwa na digrii kungeepusha vipi vifo kama taratibu za kiusalama ziliachwa? Huku ninkuhamisha goli, hoja hapa ni kwa nini polisi hawakuwajibika kuzuiia mkutano kuendelea wakati muda ulioruhusiwa umekwisha. Angekuwa mwanasiasa angeshushwa kwa tanganyika jeki hapo kwenye jukwaa

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
johnthebaptist,

Shida sio Elimu, wote wanaweza Kuwa na Elimu na wakaharibu, Mwamposa hana Elimu?
Waziri anakwepa lawama kwa kuhamisha goli. Tukio hili linahusu usalama wala sio teolojia wala mafundisho. Ingekuwa amefundisha uasi dhidi ya serikali ama mafundisho mengin potofu tungesema tuna tatizo upande wa elimu.

Nadhania ni heri wangeweka utaratibu polosi wawe na phd ili kuajiriwa labda watawajibika kusimamia usalama wa raia na mali zao. Waziri aache kukwepa lawama

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Tatizo sio dini. Tatizo ni usimamizi wa hii mikutano. Halafu kuna jambo la elimu kwa wananchi. Elimu yetu ikiwa ndogo tutaendelea na huu ujinga. Hao wenye digrii wataendelea kula darasa la saba.
 
Degree zetu hizi hizi? Hata Ph.D mashaka matupu.

Serikali iwapunguzie wananchi wake njaa ili waweze kufikiria vizuri, wasiokotwe okotwe.
Nami niliwaza ni heri wananchi ndio wapewe elimu ya digrii ili waweze ku reason kuliko kujidanganya wachungaji wawe na digrii. Hata sasa wanazo tele. Wananchi wasomeshwe ngazi ya digrii ili waweze kufanya upembuzi yakinifu (ingawa tulitarajia makanisa haya yasiwe na msomi hata mkoja).

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Waziri wa mambo ya ndani Mh Simbachawene amesema kufuatia vifo vya watu 20 kwenye Huduma ya Mwamposya huko Moshi, serikali itaangalia upya utaratibu wa kusajili hizi Huduma.

Simbachawene amesema Wachungaji wanaoanzisha Huduma za kiimani watapaswa kuwa na shahada ili kupunguza " Vibanda Imani" vilivyozagaa kila kona.

Rwanda wamefanikiwa kudhibiti Vibanda Imani kwa kutumia utaratibu huu, amesisitiza Simbachawene.

Source Clouds tv!
Nämna nzuri ya kuliweka saga hili ni kuitisha mkutano na wadau kwa maana ya taasisi zany usajiri na kuandaa rasimu ya kanuni. Sikubaliani na utaratibu za kuruhusu uanzishwaji wa makanisa yanayomilikiwa na mtuu binafsi
 
Ss unataka watanzania waendelee kupoteza maisha kwa sababu kama hizi?.aka ' vilainishi'
hilo ni tukio la ngapi toka Tanzania liwe taifa? basi moja likiua abiria wote 60 kwa hiyo unapiga marufuku mabasi tanzania? kuwa wataendelea kufa kwa mabasi??
 
Kwani tatizo ni aina ya mafunndisho au ni taratibu za kiusalama zilizopelekea vifo? Kwani kuwa na digrii kungeepusha vipi vifo kama taratibu za kiusalama ziliachwa? Huku ninkuhamisha goli,
Hapa ndipo waziri anatakiwa kujikita kutafuta ufumbuzi wa usalama mambo ya imani aachie wenyewe.Kuwa the way forward usalama uweje ili tukio kama hilo lisijirudie.Na ashirikiane na viongozi wa dini swala kuu si kujadili imani ya nani anaamini nini ni kujadili utaratibu mzuri wa usalama kwenye mikutano iwe ya kukanyaga mafuta au kukanyaga mavi ya upako
 
hilo ni tukio la ngapi toka Tanzania ipate liwe taifa? basi moja likiua abiria wote 60 kwa hiyo unapiga marufuku mabasi tanzania? kuwa wataendelea kufa kwa mabasi??
Mabasi yakipata ajali unaregulate mwendo
Sote ni mashahidi jinsi speed 80 ilivyosaidia ktk kuondoa ajali nchini
Nawapongeza wahusika kwa hilo...sana tu

vile vile ktk hili Mwamposa achukuliwe hatua na hii sekta ya dini iwe 'regulated' pia..ndo mana ya serikali kuwepo
 
Ibada gani hio ya kukimbizwa mkanyage Korie🤗
 
Manisa la AICT na wasabato wamefanikiwa sana kuwa na wachungaj wasomi. Hongera zao

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata Katoliki na Lutheran shule tupu imejaa pale

uongo mbaya elimu inakuja na ustaarabu

na vitu vya kijamii kama makanisa nadhani ni sahihi zaidi yakiwa 'Taasisi'
Kuna kua na dhana ya 'udhibiti' wa nani anafanya nini na namna ya kumudu mkusanyiko huo wa watu
 
Mabasi yakipata ajali unaregulate mwendo
Sote ni mashahidi jinsi speed 80 ilivyosaidia ktk kuondoa ajali nchini
Nawapongeza wahusika kwa hilo...sana tu

vile vile ktk hili Mwamposa achukuliwe hatua na hii sekta ya dini iwe 'regulated' pia..ndo mana ya serikali kuwepo
UNA DEAL NA PROBLEM YA SPIDI ILIYOSABABISHA AJALI INGAWA SI LAZIMA AJALI ZOTE KISA SIPIDI KUNAWEZA KUWEPO KUCHOMOKA TAIRI NK

MOSHI PROBLEM ILIKUWA USALAMA UNATAKIWA U DEAL NA PROBLEM YA USALAMA KWENYE MIKUTANO YOTE IJAYO IWEJE ILI KUHAKIKISHA KUNA USALAMA MIKUTANONI SI YA KIDINI TU BALI YOTE SI KU CONCENTRATE KWENYE NON ISSUE AMBACHO SIO MAIN PROBLEM YA VIFO VYA WATU MOSHI
 
UNA DEAL NA PROBLEM YA SPIDI ILIYOSABABISHA AJALI INGAWA SI LAZIMA AJALI ZOTE KISA SIPIDI KUNAWEZA KUWEPO KUCHOMOKA TAIRI NK U

MOSHI PROBLEM ILIKUWA USALAMA UNATAKIWA U DEAL NA PROBLEM YA USALAMA KWENYE MIKUTANO YOTE IJAYO IWEJE ILI KUHAKIKISHA KUNA USALAMA MIKUTANONI SI YA KIDINI TU BALI YOTE SI KU CONCENTRATE KWENYE NON ISSUE AMBACHO SIO MAIN PROBLEM YA VIFO VYA WATU MOSHI
NO
Inabidi twende mbali zaidi kumaliza hilo tatizo

jitahidi kutafakari factors zote na uone namna ya kuzi'control/monitor
 
Back
Top Bottom