Waziri wa mambo ya ndani Mh Simbachawene amesema kufuatia vifo vya watu 20 kwenye Huduma ya Mwamposya huko Moshi, serikali itaangalia upya utaratibu wa kusajili hizi Huduma.
Simbachawene amesema Wachungaji wanaoanzisha Huduma za kiimani watapaswa kuwa na shahada ili kupunguza " Vibanda Imani" vilivyozagaa kila kona.
Rwanda wamefanikiwa kudhibiti Vibanda Imani kwa kutumia utaratibu huu, amesisitiza Simbachawene.
Source Clouds tv!
Ingawa mimi sina ufungamano na dini rasmi yoyote, na zaidi, siamini hata uwepo wa Mungu, napenda sana kudumishwa kwa haki za kikatiba za uhuru wa kuabudu.
Kila mtu aabudu anavyotaka, ilimradi havunji sheria wala kuhatarisha usalama.
Katiba inatupa haki za kuabudu.Haki hizi ni za msingi na zina historia ndefu.
Kuweka vikwazo vya elimu ya kidunia kwenye uchungaji ni kuiminya haki hii ya kikatiba.
Sheria yoyote itakayolazimisha mchungaji awe na shahada itakuwa inaminya uhuru wa kikatiba wa kuabudu, vipi kama dini haiamini katika elimu ya kidunia? Na yenyewe ilazimishwe mchungaji wake awe na shahada?
Tunahitaji serikali iweke mazingira ya usalama ili watu waabudu kwa uhuru na usalama, hatuhitaji serikali iingilie uhuru wa kuabudu.
Kuna mstari mwembamba sana unaotenganisha mawili hayo.
Tamko hili la waziri lilitekelezwa, serikali itakuwa imeingilia uhuru wa kuabudu bila kuzidisha usalama.
Kwa sababu, hata hizo shahada hazihakikishi wachungaji hawatafanya mambo vibaya.