Simbachawene: Wako watu wanaofikiria Rais Samia hapendi Dodoma, wanamsingizia. Hana kusudio kurudisha makao makuu Dar

Simbachawene: Wako watu wanaofikiria Rais Samia hapendi Dodoma, wanamsingizia. Hana kusudio kurudisha makao makuu Dar

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Waziri George Simbachawene amesema Serikali ilifanya maamuzi ya kuhamia Dodoma mwaka 1973 na sasa taasisi zote muhimu zinakamilisha ujenzi wa majengo yake Dodoma ikiwemo Ikulu na wizara zote zimetengewa bilioni 20.

Simbachawene amesema zipo taasisi zinazosita kuhamia Dodoma na wako watu wanaofikiria Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan hapendi Dodoma kitu ambacho wanamsingizia. Amesema Rais anatenda kwa vitendo na pesa inayoingia Dodoma ni nyingi kwasababu hiyo.

Simbachawene amesema Rais Samia hana makusudio yoyote ya kurejesha makao makuu Dar es Salaam na wiki ijayo atatoa tamko kwa wale ambao bado wanasitasita kuhamia Dodoma
 
Hana kusudio hilo wakati kila siku mataa ya Kamata tunapotezewa masaa yasiopungua matatu kumsubiria atoke Airport au kwenda
 
Waziri George Simbachawene amesema Serikali ilifanya maamuzi ya kuhamia Dodoma mwaka 1973 na sasa taasisi zote muhimu zinakamilisha ujenzi wa majengo yake Dodoma ikiwemo Ikulu na wizara zote zimetengewa bilioni 20...
Off Course ni ujumbe wa kijasusi kwa Amiri Jeshi Mkuu mwenyewe.
 
Simbachawene karusha jiwe gizani kwa watu ambao hawajamuelewa basi wanatatizo kubwa la kufikri
 
Simbachawene, hiyo meza unayojaribu kutikisa ina vinywaji vya wakwe.
 
Waziri Simbachawene amesema Rais Samia hana nia yoyote ya kuyarejesha makao makuu ya serikali jijini Dar es salaam

Simbachawene ameliambia bunge kuwa Rais Samia anaupa Bajeti kubwa mkoa wa Dodoma tofauti na mikoa mingine yote

Source ITV habari
 
Back
Top Bottom