SIMIYU: Jeshi la Polisi lamkamata mtuhumiwa (mganga wa kienyeji) akiwa na fisi

SIMIYU: Jeshi la Polisi lamkamata mtuhumiwa (mganga wa kienyeji) akiwa na fisi

Sema mganga nae kazingua, kama sio muda wa kumtumia, si ilibidi amgeuze fisi wireless..yan haonekani!!!
 
maadamu jeshi limebaini viashiria vya tamaduni kutolinda utu na mali za raia nawaunga mkono ndugu zangu kwa hilo
 
Ila CCM wamezidi. Kwahiyo hizo nguo za mbogamboga walivaa saa ngapi?
Huyo mnyama awape hao TAWA waone moto wake
 
Tangu lini serikali imeanza kuamini mambo ya kichawi/ushirikina? Polisi inaaminije kuwa huyo ni fisi halisi? Mamlaka ya wanyamapori wakimchukua mnyama wao watampeleka porini akaendelee na maisha ya porini? Je kama wamechukua msukule/zombi lenye umbo la fisi wakaliaje porini hawaoni kuwa litarudi kijijini kusumbua watu? Anyway TAWA na TAWIRI ndio wenye kuthibitisha kuwa huyo ni fisi halisi au wa mchongo
Japo pengine ni nyara za serikali lakini polisi wamekurupuka. Mkuu wa mkoa Kihongosi alipofika tu ilibidi ajitambulishe kwa waganga wa kienyeji wote wa Simiyu; na naamini ataingilia kati na mganga huyu ataachiwa huru.

Fisi hawa wanaotumiwa na waganga wa kienyeji pamoja na wachawi siyo fisi halisi bali ni vivuli tu vya mambo mengine. Fisi hawa wakikutembelea usiku wanaweza kukusemesha kabisa kwa kukuita jina lako; na kwamba wamekuja kukusalimu. Inashauriwa sana kuwa usiwajibu maana ukikosea tu ukawasemesha basi kwa hakika kitaumana kama huna kinga; na utaresti ini pisi kishikaji shikaji tu.

Fisi hawa hutumiwa kama vyombo vya usafiri; na kuchukua watu ikiwemo misukule ili kuwapeleka sehemu wanakohitajika. Na ili kumiliki fisi wako kwa ajili ya shughuli hizi ni process ndefu kidogo maana inabidi utume maombi na ukubaliwe kuwa unastahili. Na hii inaambatana na kufikia cheo fulani katika rank za uchawi; na ni lazima utoe mtoto wako mpendwa au ndugu yako wa karibu kama mchango wako katika īgūngūli (jumuia) ulilomo. Hivyo ukiona mtu ana fisi wake basi tambua kuwa mtu huyo ni mchawi aliyehitimu.

Huyu mganga ataachiwa huru!
 
Ethiopia wanapiga nao stori kabsa 😃
 
Taarifa ya Jeshi la Polisi imesema Januari 24, 2025, saa kumi na mbili jioni katika Kijiji cha Kilulu Kata ya Bunamala Tarafa ya Ntuzu wilayani Bariadi, Jeshi la Polisi kupitia kikosi kazi cha kupambana na uhalifu, kilifanikiwa kumkamata Emmanuel John Maduhu (31), Msukuma na mganga wa kienyeji akiwa na mnyama huyo akiwa hai.
View attachment 3213942

“Mganga huyo alieleza kuwa anamtumia fisi huyo katika shughuli za uganga wa jadi ikiwa ni pamoja na kumtumia kama chombo cha usafiri anapotaka kupaa angani,” imeeleza.

Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Mamlaka za Wanyamapori imesema wanaendelea na uchunguzi na mara baada ya upelelezi kukamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
View attachment 3213941

Rai yangu:

1. Naomba Jeshi la Polisi lifanye msako mkali sana kutafuta wanaofuga fisi maeneo hayo, ni wazo zuri sana kuona polisi wakifanya doria nyakati za usiku haswa kuanzia saa 5 usiku mpaka majira ya saa 10 ili kupata wavunja sheria kama huyu mganga. Mikoa ya Simiyu, Shinyanga pamoja na baadhi ya viunga vya Tabora kumekuwa na tatizo hili.

2. Mambo ya kufuga fisi pamoja na kutumia fisi kama usafiri yamekuwa yakisemwa sio leo wala jana, ni mambo ambayo toka zamani watu wamesema, sio wapita njia wa Maganzo wala Tinde, wengi wamesimulia matukio ya kukutana na fisi akiwa anaendeshwa na mtu tena kwa mwendokasi wa kasongo. Badala ya kumkamata toeni elimu kwa watu watumie sayansi zao vyema. Leo mmemkamata huyu kwa kufuga fisi, je mkienda Ukara mtakamata wangapi kwa umiliki na ufugaji wa Mamba? Mganga hana kosa muacheni, Emmanuel hana kosa lolote.

3. Kuna matukio mengi yanahitaji utatuzi wa jeshi la polisi sio kwenda kumkamata mganga na kumfungulia mashtaka ambayo mnajua kabsa wengi wanafanya. Wekeni kambi usiku sehemu tajwa mkaone fisi zinavyotembea mwendokasi wa engine V16. Mwanamalundi angekuwa hai basi naye angekuwa matatani kwa mujibu wa Polisi na Mamlaka za Wanyamapori.
Huyo Mganga nae kafeli kwanini asingewapiga Upofu hao askari au awaoteshe mabusha ili wawe na adabu
 
Back
Top Bottom