Simiyu: Kihongosi amzawadia Msaidizi wake Pikipiki kwa kazi nzuri

Simiyu: Kihongosi amzawadia Msaidizi wake Pikipiki kwa kazi nzuri

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Kenani Kihongosi amempatia zawadi ya pikipiki mpya aina ya SAN LG Msaidizi wake wa Ofisi (PS) Florenciana Kagya, kutoka na kazi nzuri anayofanya na kujituma katika ofisi yake.

Kihongosi amesema kuwa ameamua kutumia mshahara wake kumnunulia msaidizi wake huyo zawadi ya pikipiki, ambapo alieleza mbali na kujituma amekuwa mshauri na mama mlezi kwake tangu afike katika ofisi hiyo.

Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa kama kiongozi na kama mtoto kwa msaidizi wake huyo, anao wajibu wa kuwasaidia watumishi wenzake na kuwatia moyo katika majukumu yao ya kila siku.

Amebainisha kuwa anatambua kuwa zawadi hiyo ambayo ameitoa kwa msaidizi wake ni sadaka na itakwenda kumsaidia katika shughuli zake za kila siku na kuongeza hari ya utendaji kazi wake.
 
Ni jambo zuri lakini angeweza kuitoa kimya kimya pasipo kuita waandishi wa habari.
 
Ukishatoa kitu mbele ya kamera huo sio msaada tena, unafanya hivyo kwa malengo yako mengine.
 
Back
Top Bottom