Simiyu: Lori laua wanne na kujeruhi 15, Rais Samia atoa pole

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
267
Reaction score
1,014
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa pole kwa wananchi wa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu kwa vifo vya watu wanne kufuatia ajali ya lori aina ya Scania iliyotokea katika Kijiji cha Mwamishari Juni 16 saa 3 usiku, akisema watu hao walikuwa kwenye usafiri wa kwenda kwenye mkutano wake.

Kabla ya kufika kwenye mkutano huo, Rais Samia ambaye yuko kwenye zaiara ya siku tano mkoani Simiyu, pia aliwatembelea majeruhi waliolazwa katika hospitali ya wilaya hiyo.

Hata hivyo, taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu leo Juni 17 imesema mbali na vifo hivyo, ajali hiyo imesababisha majeruhi 15, ambapo 13 kati yao ni wanaume.
"Ajali hiyo ilisababishwa na uzembe wa dereva kwa kushindwa kulimudu gari akiwa kwenye kona kali. Miili ya marehemu imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu," imesema taarifa hiyo.

Pia soma ~ Watu wanne wapoteza maisha katika ajali, Polisi Wasema walikuwa wanatoka kwenye zoezi la chanjo ya mifugo na utambuzi


Your browser is not able to display this video.
 
Jini subiani linazidi kunyonya damu za Watanganyika.
 
jini CCM limepata damu tayari limeshiba
 
Na Bado, hadi October,tutamzika Saa100
 
Masikini humo unakuta kuna CHAWA kaded kaacha familia yake yenyewe imechoka alikuwa anaenda kumshangilia mama ili alipwe 15k ya kibaba cha unga na dagaa. Mungu atusaidie
 
Wekeni picha!! Na video
 
Tatizo wananchi wengi hawana elimu ya kutambua ni jinsi gani wanasiasa wanaweza kutumia akili zao vibaya. Onasombwa na lori kiboya kwani umekuwa mzigo? Yale mabasi yao ya kijani yanafanya nini, yanasubiri kampeni? Unabebwabebwa bure bila posho ya kushiba, huo ni uendawazimu. Mwananchi tulia fanya shughuli zako acha kubebwa na upepo upitao utaumia bure
 
Yafe yote nani kawalazimisha kwenda huko
 
Kuna baadhi ya watu hii ni taarifa njema kwao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…