Simiyu: Mkuu wa Wilaya ya Busega: Nimepigwa mawe wakati wa Maandamano, tumewakamata Watu 108

Angetakiwa avunjwe taya huyu
Au awe mochwari
 
Mwenyekiti anadai alitoa taarifa na wakaambiwa wasubiri viongozi kutoka wilayani....mkuu wa wilaya anasema hajui lolote, dah
 
Kuna kitu kinaendelea..hao wananchi mpaka wamefanya kitu kama hicho lazima kuna jambo....Inashangaza sana kiongozi anasema hana taarifa...yajao yanatisha sana...
 
Failed state, unakamata vipi watu 108, hayo ni matumizi mabaya ya resources za nchi.

Jeshi la polisi acheni uvivu, jikiteni katika kufanya uchunguzi na kubaini wahusika haswa ni kina nani, acheni kurahisisha mambo
 
Wakati baadhi ya Wananchi wakikiri kuwa kuna Watu kadhaa wanahofiwa kufariki kutokana na kupigwa risasi na Polisi wakijaribu kuwatawanya kwenye maandamano yaliyofanywa na Wananchi huko Busega Mkoani Simiyu leo, imethibitika kuwa Mkuu wa Wilaya ya Busega Faiza Salim pamoja na Maofisa wengine wamejeruhiwa kwa mawe na Wananchi hao.


@AyoTV_ imeelezwa kuwa Wananchi walimrushia Mkuu huyo wa Wilaya mawe wakati akiwasogelea kwa nia ya kuwasikiliza ambapo hawakutaka Kiongozi huyo kufanya chochote na kuanza kumrushia mawe yaliyopelekea kujeruhiwa kwenye ubavu na mgongoni huku Maofisa wengine aliokuwa ameambatana nao ambao ni Kamanda wa Zimamoto Simiyu na Kaimu Afisa wa TAKUKURU Simiyu wakijeruhiwa kichwani na kupelekea kushonwa nyuzi.


Kwa sasa hali zao zinaendelea vizuri na wameruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kupata matibabu.


Wananchi wa Busega waliandamana leo hadi Kituo cha Polisi baada ya kuchoshwa na kushamiri kwa matukio ya Watoto wao kupotea katika eneo la Lamadi bila Polisi kuchukua hatua za kuridhisha kudhibiti matukio hayo. #MillardAyoUPDATES


View: https://x.com/millardayo/status/1826314931727466877?t=QgmZBVl1PdkVwqECySfnXA&s=19
 

Kuna mwanzo wa ngoma..hapo DC
 
Jeshi la polisi lichukulie hilo suala kwa uzito,wananchi wameghadhibika,wanalipa kodi ili walindwe wao na mali zao,halafu watoto wanapotea.
Walishuhgulikie hilo suala kwa weledi.
 
Wangekukata na kichwa kabisa
 
Hilo nalo ni neno.
 
Washughulikiwe wote waliotaka kuvamia Polisi,kukiteka na kuchukua sheria mkononi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…