SIMIYU: Mmoja ajinyonga mpaka kufa akiwakimbia RC Kafulila na Rais Samia

SIMIYU: Mmoja ajinyonga mpaka kufa akiwakimbia RC Kafulila na Rais Samia

Umeshamuamini marehemu tayari,kwa ujumbe ambao huna uhakika Kama ni wa marehemu
Sijahukumu. Vyombo vya upelelezi vipo na vya kutoa haki vipo.
Hapo ndio pa kuanzia.
Inawezekana ikawa kama ya yule polisi wa Mtwara au bwana Mwijabe wa Hazina.
 
Aulizwe aliyeandika huo ujumbe.

Hakuna mwenye hakika kama marehemu ndie mwandishi na kajiua.

Nchi zilizoendelea, zenye vyombo vya wachunguzi weledi, na raia wasomi, na wana habari wataalam, wakikuta kitanzi shambani hawakimbilii kusema marehemu kajinyonga, bwana ametoa, bwana ametwaa, chanzo Kafulila, twendeni tukaswali halafu tukazike. Hell freaking no!
Uchunguzi muhimu hapooo
 
Katumbili katawanyoosha, haka kajamaa naona kana moyo wa uzalendo aise
Tumbili ni tumbili tu. Hukumbuki kalinunuliwa kwa Bei ya jioni kwenye utawala wa mtu yule?
Kujipendekeza kwingi.
 
Aulizwe aliyeandika huo ujumbe.

Hakuna mwenye hakika kama marehemu ndie mwandishi na kajiua.

Nchi zilizoendelea, zenye vyombo vya wachunguzi weledi, na raia wasomi, na wana habari wataalam, wakikuta kitanzi shambani hawakimbilii kusema marehemu kajinyonga, bwana ametoa, bwana ametwaa, chanzo Kafulila, twendeni tukaswali halafu tukazike. Hell freaking no!
Wewe unatakaje?
 
===
Mr Daniel Jilala mwenye umri wa miaka43 ambaye ni katibu wa chama cha msingi cha Ushirika AMCOS,

Mkazi wa kijiji cha Sulu wilaya ya Maswa mkoani Simiyu amekutwa amejinyonga kwa kamba kwenye mti jana jioni Mei27, 2022,

Bwana Jilala ameacha ujumbe wa simu( sms) aliomtumia mmoja wa afisa wa TAKUKURU ulioshiria kuwa ni muhanga wa opareshen inayoendeshwa na RC Kafulila wa Mkoani Simiyu,

RC David Kafulila ameanzisha operesheni hii ili kusafisha uozo ndani ya vyama Ushirika,

Mtakumbuka oparesgen hii ina baraka za Rais Samia Suluhu Hassan,

Simu ya marehemu imekutwa na ujumbe aliomtumia kwa mmoja wa maofisa TAKUKURU wilaya Maswa mwenye namba 0622591912 uliosomeka

" NIMEAMUA KUJIUA KWASABABU SIJASAIDIWA , NAOMBWA RUSHWA KILA SIKU NA AFISA USHIRIKA BUDODI KUWA ANAWAPELEKEA TAKUKURU MKOA LAKINI SIONI MATUMAINI YA SUALA LANGU NA INAELEKEA NITAFUNGWA, SASA SIONI SABABU KUISHI KWANI SIJUI WANANGU WATAISHIJE IKIWA NITAFUNGWA"

April 4, 2022 akigawa pikipiki Dodoma kwa maofisa ugani nchi nzima tukio lilioandaliwa na wizara ya Kilimo,

Rais Samia Sukuhu Hassan alimwelekeza Mkuu wa Mkoa Simiyu, Mhe David Kafulila kuendelea kudhibiti wizi wa pembejeo za pamba na michezo michafu kwenye vyama vya ushirika na Ushirika..

" Nakuagiza Kafulila, endelea kuwakaba, najua wapo ambao mliowafungulia mpaka kesi za uhujumu uchumi kwa wizi wa madawa ya pamba. Nasisitiza endelea kuwakaba wezi wa pembejeo na ushirika wote tena kwa hatua kali mpaka wazijue rangi zangu" aliagiza Rais Samia Suluhu Hassan,

Katika utekelezaji huo RC Kafulila aliwaondoa maofisa ushirika wote ngazi ya wilaya na kuelekeza wapangiwe kazi zingine wilayani kwani ni sehemu ya madhaifu ya usimamizi wa ushirika na hujuma kwa wakulima pamba.

Mpaka sasa vyama vya msingi 182 kati ya 335 vimefanyiwa uchunguzi na TAKUKURU ambapo nyingi zimerejesha fedha ama za wakulima au wanunuzi na kubaki AMCOS 37.
Duh!
 
Jamani tuwe tunaongea matatizo yetu na watu tunaowaamini inasaidi kutojitoa uhai km huyo karani
 
Back
Top Bottom