Simiyu: Mwili wa mtu waokotwa kwenye sandarusi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mwili wa kijana Ezekiel Boniphace Mangu (30) mkazi wa Kata ya Somanda Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu, umekutwa umewekwa kwenye Sandarusi na kufunikwa na shuka kichakani.

Mashuhuda wa tukio hilo wanasema kijana huyo aliyekuwa akifanya kazi ya ulinzi alipotea usiku wa Desemba 31/2022.

Kamanda wa Polisi mkoani Simiyu, ACP Blasius Chatanda, amesema kijana huyu amefariki kwa kunywa pombe huku baadhi ya wananchi wakivitaka vyombo vya usalama kuongeza uchunguzi zaidi

Chanzo: EATV
 
Polisi wa Tanzania wakati mwingine jama mijusi. Maelezo rahisii alipoona pombe zimemzidia akajifunika zake shuka akajigeuza nafaka akjiingiza kwa sandarusi. Shikamoo TZ.
 
Sandarusi ni kitu gani jamani naombeni mnitafsirie kwa neno jingine.
 
Jamani Sandarusi ni Kiroba jamani watu wa daresalam nawajulisha kabsa msije mkauliza sandarusi ni nini?
 
Mwili wa kijana Ezekiel Boniphace Mangu (30) mkazi wa Kata ya Somanda Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu, umekutwa umewekwa kwenye Sandarusi na kufunikwa na shuka kichakani.

Mashuhuda wa tukio hilo wanasema kijana huyo aliyekuwa akifanya kazi ya ulinzi alipotea usiku wa Desemba 31/2022.

Kamanda wa Polisi mkoani Simiyu, ACP Blasius Chatanda, amesema kijana huyu amefariki kwa kunywa pombe huku baadhi ya wananchi wakivitaka vyombo vya usalama kuongeza uchunguzi zaidi

Chanzo: EATV
Si hata yule wa mabus naye aliishia kwenye viroba. Mwanza /Simiyu nani kawafundisha hayo?
 
Back
Top Bottom