Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Mkuu wa mkoa wa Simiyu Kenani Kihongosi amewaasa wakazi wa mkoa huo kuendelea kujitokeza kwa wingi katika vituo vya kupigia kura katika mitaa yao ili kuchagua viongozi watakaowaongoza katika mitaa yao.
Akizungumza baada ya kupiga kura katika mtaa wa Sesele uliopo kata ya Nyakabindi wilayani Bariadi mkoani humo mkuu huyo wa mkoa pia ametoa maelekezo kwa wananchi kutosalia vituoni baada ya kupiga kura.