Simiyu yavunja rekodi ukusanyaji wa Mapato 2021/22

Simiyu yavunja rekodi ukusanyaji wa Mapato 2021/22

Mkoa wa Simiyu wafunga mwaka wa fedha unaoishia Juni30, 2022 kwa kuvunja rekodi ya makusanyo ya Halmashauri,

Simiyu imekusanya 14.2bn sawa na asilimia 108% kulinganisha na makusanyo ya 10.9bn sawa na asilimia 76% mwaka ulioisha Juni30, 2021.

Huku Maswa ikiongoza kwa makusanyo ya asilimia 125% ikifuatiwa na Meatu na Bariadi vijijini zenye asilimia 110% kila moja.

Itilima wao waliokuwa wamwisho kimapato wakati wote wamekusanya 106%

Huku Bariadi Mjini yenye asilimia 103% huku Busega ikifunga kwa asilimia95.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe David Kafulila ametoa taarifa hiyo akiwapongeza wakurugenzi wote wa Halmashauri chini yake kwa kuhakikisha Mkoa unaendelea kuonesha ufanisi katika makusanyo na matumizi.

View attachment 2287122
#SIMIYUTUKO TAYARI KUHESABIWA WEWEJE?
Safi sana sio nyie tuu Mikoa kadhaa imefanya hivyo ikiwemo Mbeya..

Na mwaka wa Fedha uliomalizika, Tamisemi wamevuka malengo yao ya makusanyo kwa mara ya kwanza..

Sera za Rais Samia Kufungua Nchi zimelipa.
 
Wanajiwekea budget ndogo ukilinganisha na vyanzo vyao vya mapato alafu unasema wavunja record, ni sawa wewe ujiwekee mauzo ya duka lako kwa siku ni 20. Lafu duka lenyewe ualisia mauzo ni elfu hamsini kwa siku , ukipata elfu hamsini unajisemea umevunja records wakati huo ndio ualisia
Miaka iliyolita kwa nini hiyo bajeti ndogo waliyojiwekea hawakuifikisha?
 
..hata mimi nashangaa ni kitu gani kimesababisha MLIPUKO/MFUMUKO wa ukusanyaji mapato mkoani Simiyu.

..Je, kuna CHANZO KIPYA cha mapato ambacho hakikuwepo miaka iliyopita na kimeanza kuchangia mwaka huu?

..Je, kuna MFUMO MPYA wa kukusanya mapato ambao umeanza kutumika mwaka huu na umeziba matundu ya miaka iliyopita?

Je, kuna ongezeko la MAVUNO au mapato ya wananchi kwa kiwango kisicho cha kawaida kulinganisha na miaka iliyopita?

..Ukusanyaji wa mapato ni jambo jema, lakini ni vema zaidi tukajua ongezeko hilo linatokana na nini. Tukiweza kufanya hivyo tutakuwa ktk nafasi nzuri ya kuendelea kukusanya mapato hayo, au hata hata kuongeza makusanyo.
Pesa zilikuwa zinaliwa na waambata wa Mwendazake na pia biashara zilikufa nyingi kipindi hicho ila sasa zimefufuliwa..

Kwani huoni hata Bei ya pamba mwaka huu ni kubwa kuliko miaka mingine? The same to Mchele na Mafuta/alizeti.
 
Nilitaka nikuite jina fulani nikaamua kukusamehe. Kwa hiyo mtu akikupa chabgamoto anakuwa mwizi, mjinga kama wewe au?
Hakuna changamoto uliyotoa hapo zaidi ya kijiba cha roho..

Hapo si alikuwepo mliyemuita wa Ukweli bwana Mtaka sasa kamuulize kwa nini alishindwa atakupa jibu moja tuu kwamba Jiwe alikuwa hasomeki.
 
Back
Top Bottom