TANZIA Simon Amon Mwanguku, aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara (1983 -1992), Afariki Dunia

TANZIA Simon Amon Mwanguku, aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara (1983 -1992), Afariki Dunia

MagerezaTanzania

New Member
Joined
Jun 1, 2023
Posts
2
Reaction score
19
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Mzee Ramadhani Nyamka anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara kuanzia Mwaka 1983 hadi 1992 (Pichani), Simon Amon Mwanguku kilichotokea leo Alfajiri tarehe 28 Julai, 2024 katika Hospitali Kuu ya Jeshi la Magereza, KMKGM Ukonga, jijini Dares Salaam.

Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Familia linaendelea kuratibu shughuli zote za mazishi ya Marehemu.

Msiba upo nyumbani kwa Marehemu Segerea, Migombani.

IMG_20240728_153340_785.jpg

==================
Simon Amon Mwanguku ni nani?

Amezaliwa Tukuyu katika Kijiji kinaitwa Bujenga huko mkoani Mbeya mwaka 1938. Alianza Shule ya Masoko mwaka 1948, shule hiyo ilikuwa kilomita kadhaa kutoka Tukuyu, karibu na Ziwa liitwalo Masoko. Alisoma hapo kwa tokea 1948 hadi 1951.

Baadaye alienda Mpuguso Middle School, shule pekee iliyokuwa inaunganisha wanafunzi wa Rungwe nzima. Wakati ule Rungwe ilikuwa ni pamoja na Ileje, Kyela, na sasa Halmashauri ya Busokelo.

Baada ya Mpuguso Middle School alikwenda Malangali mkoani Iringa mwaka 1954 na mwaka 1960 alimaliza Darasa la 12.

Wakati akiwa Malangali, alikutana na watu wawili ambao walikuwa ni inspekta wa polisi, kwa udadisi yeye na wenzake wakawauliza kuhusu utaratibu wa kujiunga na Jeshi la Polisi. Na kilichowavutia hadi kuuliza ilikuwa ni ‘smartness’ ya mabwana wale.

Baadaye alikwenda kujiunga na mafunzo na mwaka 1961 alijiunga na Jeshi la Magereza. Alipita vyeo kadhaa katika jeshi hilo lakini safari yake ya uongozi ndani ya jeshi hilo ilianza mwaka 1967, mkoani Morogoro.

SAFARI YA UONGOZI
  • Mkuu wa Gereza Wami – (1967)
  • Mkuu wa Gereza la Molo, Sumbawanga (1967 – 1976)
  • Mkuu wa Gereza Moshi (1976-1979)
  • Kamishna wa Jeshi la Magereza (1979 – 1983)
  • Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza (1983 – 1992)
 
Inna lillah wainna ilaihyi rajiun.
Apumzike kwa Amani mzee wetu.
 
Poleni Sana Jeshi Na Watanzania Wote
Apumzike Kwa Amani Kamanda


Pia Magereza Tanzania
Hongereni Kuwa Member Hapa JF, Karibuni Sana Sana Tuijenge Tanzania Yetu
 
Back
Top Bottom