Sioni ubaguzi wowote dhidi ya Msuva! Msisahau Samatta katoka Simba, kaenda TP Mazembe! Tanzania tunaifahamu sana TP Mazembe kulinganisha na timu ambayo Msuva alienda ambayo hata hapa tukiambiana tuitaje, watu tutapata taabu! Na uzuri zaidi, Samatta akawa staa pale Mazembe, kiasi kwamba umetaka usitake, utamjua tu labda mtu uwe hufuatilii kabisa soka!! Kwa upande mwingine ligi ya Morocco hatuijuia, na ukichanganya na kile Kiarabu chao, ndo kabisa!!
Lakini la pili, baada ya Samatta kwenda Belgium, pale napo akawa staa kama ilivyokuwa DRC!! Kacheza Club Bingwa; sasa utashangaa media za Bongo kumpa coverage!! Mbaya zaidi, miaka miwili tu baadae, Waingereza kama kawaida yao kwa kelele, kila msimu mara oh Samatta, mara oh Everton, mara Chelsea yammezea mate Ali! Ni hizi kelele za waingereza ndizo pia zilikuwa zinanaswa na media za Tanzania! Kwa upande wa Msuva, hata hiyo enda yake Benfica, hatukusikia kwa sababu media za Ureno hazina kelele kama zile za Uingereza!! Kwahiyo Msumva katoka kwenye ligi tusiyoifuatilia wala kujua lugha yake, na kaendaa kwenye ligi ambayi sio wapiga kelele kama UK, na pia hatuifahamu lugha yao!! Na hapa nikukumbushe tu kwamba, hata enzi za David Beckham, kelele za Waingereza mtu zingeweza kumfanya aamini Beckham ndiye mchezaji bora kabisa duniani kuwahi kutokea!
Huyo huyo Msuva kama ingekuwa alinyemelewa na club za EPL hata kwa uongo uongo tu, ungezisikia kelele za media za UK ambazo media za TZ wangezidaka tu!! Ni hizi kelele za hawa Wakoloni ndizo ambazo wameturithisha hadi Wabongo!! Ka-Samatta ketu kamoja toka kwenye ligi dhaifu Ulaya alikuwa anatufanya tujimwambafai hata mbele ya Kenya wenye wachezaji ligi ngumu zaidi kulinganisha na ile ya Belgium!