Simon Msuva amesajiliwa Benfica ya Ureno

Ajibu nilishamuandikia uzi toka wakati yupo yanga kabla hajarudi huko anapopaita nyumbani.
 
Sioni ubaguzi wowote dhidi ya Msuva! Msisahau Samatta katoka Simba, kaenda TP Mazembe! Tanzania tunaifahamu sana TP Mazembe kulinganisha na timu ambayo Msuva alienda ambayo hata hapa tukiambiana tuitaje, watu tutapata taabu! Na uzuri zaidi, Samatta akawa staa pale Mazembe, kiasi kwamba umetaka usitake, utamjua tu labda mtu uwe hufuatilii kabisa soka!! Kwa upande mwingine ligi ya Morocco hatuijuia, na ukichanganya na kile Kiarabu chao, ndo kabisa!!

Lakini la pili, baada ya Samatta kwenda Belgium, pale napo akawa staa kama ilivyokuwa DRC!! Kacheza Club Bingwa; sasa utashangaa media za Bongo kumpa coverage!! Mbaya zaidi, miaka miwili tu baadae, Waingereza kama kawaida yao kwa kelele, kila msimu mara oh Samatta, mara oh Everton, mara Chelsea yammezea mate Ali! Ni hizi kelele za waingereza ndizo pia zilikuwa zinanaswa na media za Tanzania! Kwa upande wa Msuva, hata hiyo enda yake Benfica, hatukusikia kwa sababu media za Ureno hazina kelele kama zile za Uingereza!! Kwahiyo Msumva katoka kwenye ligi tusiyoifuatilia wala kujua lugha yake, na kaendaa kwenye ligi ambayi sio wapiga kelele kama UK, na pia hatuifahamu lugha yao!! Na hapa nikukumbushe tu kwamba, hata enzi za David Beckham, kelele za Waingereza mtu zingeweza kumfanya aamini Beckham ndiye mchezaji bora kabisa duniani kuwahi kutokea!

Huyo huyo Msuva kama ingekuwa alinyemelewa na club za EPL hata kwa uongo uongo tu, ungezisikia kelele za media za UK ambazo media za TZ wangezidaka tu!! Ni hizi kelele za hawa Wakoloni ndizo ambazo wameturithisha hadi Wabongo!! Ka-Samatta ketu kamoja toka kwenye ligi dhaifu Ulaya alikuwa anatufanya tujimwambafai hata mbele ya Kenya wenye wachezaji ligi ngumu zaidi kulinganisha na ile ya Belgium!
 
ni kweli mkuu uyasemayo lakn tuwe na utaratibu wa kuwatia moyo wachezaj wetu sio had media za nje zimuongelee mtu nao ndio wadakie tuanze wenyewe kwa hyo akina shafi na eddo had wasikie media za nje ndio wawatembelee wachezaj wetu mkuu? Tukiona mafanikio ya nakaribia na media nazo znajifanya ukaribu kwa mchezaji
unadhan wanapoenda huko belgium wanaenda bure kuna kias kama mchezaj anatomboka kumsaidia mwanahabar yaweza kuwa hela ya hotel na chakula au hata tiket ya ndege wanalipiwa

mkuu hawa wachezaj n ndugu zetu watoto watoto wetu au rafk zetu wanatuambia mengi juu ya hawa waandish makanjanja au opportunist
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huna unalolijua, unaongozwa na chuki na wivu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Elimu bila kipato ni ujinga.kwani asipocheza EPL wewe utapungukiwa au utafaidika Nini?
Unajua maana ya ujinga!?? Ujinga ni ignorance ambao 100% umekujaa kichwani. Yaani mpaka unachobishana hukijui..!! Nani alikuambia kutokuwa na kipato ni ujinga!?? Halafu unaniambia me nna elimu bila kipato wakati hunijui..!!

Hapo me dhamira yangu haikuwa kuji-mwambafy,nilikuwa najibu hoja yako ya kunizidi kila kitu. Kwenye majibu yangu,sikutaja elimu tu,nimetaja hadi Umri lkn kwa vile ww ni JUHA umeona elimu.

Mbwana sisi tunaomkosoa pengine ndo tunampenda zaidi kuliko ninyi bendera..Sheria na kanuni za kucheza ligi kuu ya England siyo mchezo..kwa mchezaji anayetoka kwenye nchi kama ya kwetu.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Njia ya msuva na samatha tofauti kabisa ,samatha kaanza vizuri mno kitakwimu na team kaenda Tp kawa mchezaji bora africa kwa wachezaji wa ndani ,club bingwa top scorer ,club bingwa 2,kaenda genk kabeba ubingwa na kutengeneza ufalme ,msuva anapambana tu,team aliyokwenda baada ya kutoka yanga hata kucheza club bingwa haiwezi kisha kanunuliwa benfica kapelekwa olympiakos sasa huko anatakiwa kupambana apate namba tumtakie mafaniko ,ila takwimu na team zinambeba samatha hata ukimdis hilo liko wazi,leo hii samatha angekuwa na wakala aliyenaye kwa sasa kitambo ungemuona laliga,ligue 1,epl .Takwimu hazidanganyi,Namjua dr Tibo ndio master mind nyuma ya msuva pamoja na bidii ya kijana
 
Matunda ya awamu ya tano hayo chini ya jemedari JPM , kwa nini awamu nyingine hayakutokea hayo bado hamjiulizi tu?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

Ungekuwa mfuatiliaji mzuri ungejuwa kuwa Eddo Kumwembe ameshawahi kwenda Morocco kwa ajili ya Msuva na akawa na mfululizo wa makala karibu wiki nzima. Sio kwamba Msuva hajaandikwa, kaandikwa kwa kiwango kilichostahili hasa kwa sababu kwa vyovyote vile asingeweza kuwa promoted kuliko Mbwana Samatta kwa kucheza ligi ya Morocco, tena katika timu ambayo isiyo na jina kubwa sana na akiwa hajabeba ubingwa wa nchi achana na ule wa Africa.
 

Mchango maridhawa kabisa
 
Hongera zake.Anajituma sana anapokuwa na Timu ya Taifa tofauti na yule mwenzake
 
Kweli aliyeroga waTz kafa kitambo.Awamu ya 5 ndiyo imemlea na kumfikisha hapo,kazaliwa leo na kuanza soka leo au 2015? Hakika usiombe ukoswe "maono".
We nawe na wenzako wengine muwe na akili ya kuelewa sarcasm.
Shule mnaenda kukua sio!?
 
We nawe na wenzako wengine muwe na akili ya kuelewa sarcasm.
Shule mnaenda kukua sio!?
sarcasm au sokoism? Mtu alivyokomaa huwezi fikiria kuwa alimaanisha kejeli. Akili za hao wanazijua wao tu na jiwe lao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…