Simon Msuva kubali ukweli, wewe soka la kimataifa basi!

Simon Msuva kubali ukweli, wewe soka la kimataifa basi!

Kwanza niseme Ninamuheshimu sana Saimon Msuva kama mchezaji na pia kama binadamu, nidhamu yake ndani na nje ya uwanja ni ya kiwango cha juu sana.

Lakini pia ni mchezaji ambae kila anapovaa jezi ya timu yetu ya taifa hujituma kwa moyo wake wote na passion yake juu ya mchezo wa soka huwa anaionyesha hata katika soka lake ngazi ya vilabu, na niseme wazi kwangu binafsi msuva Ƥtabaki kuwa mmoja wa wachezaji nyota wa muda wote wa taifa letu.

Lakini kwa bahati mbaya mchezo wa soka unaenda na nyakati na umri, soka sio kama kuendesha gari kitu unachoweza kukifanya mpaka uzeeni, soka ni mchezo wa muda mfupi na uwezo unapoanza kushuka huwezi kujificha sababu mpira unachezwa hadharani.

Kila nikimtazama sSaimon Msuva wa sasa simuoni Msuva wa miaka 10 nyuma achilia mbali kupotea kabisa kwa Msuva wa mwaka mmoja nyuma, jamaa ameshuka sana kiwango kitu pekee alichobaki nacho ni kasi isiyo na faida, yaani anapokuwa uwanjani ni sawa na mbwa koko anaezunguka zunguka asijue nini cha kufanya.

Nafikiri club ya Js kabyle ya Algeria walikuwa sahihi kumvunjia mkataba na kwauwezo wake wa sasa simuoni akicheza Ulaya au club kubwa za nje ya nchi kwa mafanikio tena kama ambavyo amekuwa akijinasibu kwamba yeye kucheza bongo bado sana.

Saimoni Msuva, umri haudanganyi kaka yangu, mimi nakufahamu nje ndani, umri wako halisi ni miaka 38, kinachokufanya uwe angalau na nguvu za kukimbia ni nidhamu yako juu ya mchezo wa soka na namna unvyoutunza mwili wako, lakini kiuchezaji kwa sasa sioni kama unaweza pata namba hata kikosi cha kwanza cha Singida fountain gate, achilia mbali Azam fc au kwa miamba ya soka toka kariakoo Simba sc na sisi Dsm Yanga africa.

Msuva naomba ukubali kuwa wakati ni ukuta na nachokushauri kwa sasa tafuta timu uarabuni ukapige pesa zako mwisho kisha utulie sababu kama Yanga sc au simba sc wakikusajili watakuwa wamejiingiza hasara, lakini nawewe utapata aibu ya mwaka, sababu yatakutokea kama yaliyomkuta Thomas ulimwengu pale singida fc, alinyanyua mabega juu lakini ameishia kuwekwa benchi na habib Kyombo.

Msuva sisi kama Yanga kwa sasa haitufai na sidhani kama makolo nao wanaweza kukuhitaji, na soka la kimataifa hutoliweza tena lakini unaweza fanya JANJA kama ya sawadogo ukapata dili lako la Mwisho.
Kila lakheri msuva[emoji2772]
Hapo wakati mpo kitandani unamuuliza umri wake alikuambia kiroho safi. Leo amekuacha unakuja anika umri wake. Wanawake..... Hatari sana nyie.
 
Hapo wakati mpo kitandani unamuuliza umri wake alikuambia kiroho safi. Leo amekuacha unakuja anika umri wake. Wanawake..... Hatari sana nyie.
Naona umeamua kunitusi bila sababu mkuu wangu. Uhuru wa maoni uko wapi 😁?
 
Familia yako utailisha wewe Mkuu? Muache apambanie kombe, ghorofa lake pale Geza bado hajamaliza vizuri
 
Naona umeamua kunitusi bila sababu mkuu wangu. Uhuru wa maoni uko wapi 😁?
Daaah.... Pole sikudhani ni wewe. Anyway.... Nisamehe tu nikikutana na watu wastaarabu hivi moyo wangu unaumia sana.... Tupo pamoja. Wewe ni mwanaume. Wangekuwa wale wengine ningeyaoga ile mbaya... Halafu ngekuwa nacheka tu.
 
Msuva na Karim Benzema ni kama mtu na mkewe siku hizi ni wameisha hatari. Tena kheri hata ya msuva anajikakamua huyo benzema wa uarabuni ndo Uozo mtupu anakula hela za Dizeli(mafuta) bure kabsa.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
ushauri mzuri, arudi amalizie soka na uto.
 
Back
Top Bottom