GE2025 Simon Sirro ndio Mfano wa Polisi Tanzania? Je, Polisi wote ni CCM?

GE2025 Simon Sirro ndio Mfano wa Polisi Tanzania? Je, Polisi wote ni CCM?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Ila kiukweli hii ni kinyume na sheria kwa sasa watu wanavunja sheria waziwazi
 
View attachment 3425585

Huu ndo uhalisia wa Polisi wa Tanzania.

Wakivua Sare za Polisi ndo unaona sare yake halisi.

Je, Sare ya jeshi la Polisi huwa inatumika kuhadaa Watanzania?

Hapa ni aliyekuwa IGP Mkuu wa Mapolisi wote Nchini baada ya kuvua sare ya Polisi

Ndo maana kila siku tunapigwa Virungu vya ugoko na Polisi tena wanatupiga ili tufe sio tupone.

Saa nyingine nawaza, Ukute ni UVCCM wamevalishwa Sare za Polisi watushughulikie🤣🤣
Policcm
 
Ila kiukweli hii ni kinyume na sheria kwa sasa watu wanavunja sheria waziwazi
Sheria ipi iliyovunjwa?
Ni usalama wa Taifa pekee, kwenye Sheria yao ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2023, ndio imepiga marufuku DGIS kuteuliwa nyashifa nyingine.

Wengine wote:
1)CDF
2)IGP
3)CGP
4)CGI
5)CGF

Sheria haijawabana hivyo wana haki kwa mujibu wa katiba, kuchagua na kuchaguliwa pamoja na kuteuliwa kwenye nyashifa nyingine
 
Imagine mkuu wa police nchini ni kada mwandamizi wa chama Tawala, halafu eti ndio wabongo mtegemee atakuwa na political neutrality anapokuwa ana deal na seke seke za uchaguzi? Hakuna kitu kama hicho.
 
Kila mtanzania ana haki ya kuwa mwanachama chama cha siasa anachokipenda.
Mkuu wa mkoa anaongoza wananchi wa vyama vyote na wasiokuwa na vyama.

Si sawa kujitambulisha kama mkereketwa wa chama fulani...!
 
Hivi nyie wenzangu mmeelewa hizo kura?

Kura halali zilizopigwa ni 1418 na washindi wawili juu kila mmoja kapata kura elfu moja mianne na ushee!

Ila ccm dah!
 
Mkuu wa mkoa anaongoza wananchi wa vyama vyote na wasiokuwa na vyama.

Si sawa kujitambulisha kama mkereketwa wa chama fulani...!
Unachokisema ni sawa japo hali halisi inapingana na mtazamo huo
 
unaelewa kinachojadiliwa hapa au unapuyanga tu? unaweza ukawa mwanachama wa TLP Kisha ukawa mkuu wa idara huko halmashauri?
 
Tuwaige nchi za kiarabu.Kiongozi mmoja tu, hamna vyama.Mabilioni ya uchaguzi yanajenga barabara na madawa hospitali.
Hilo gumu upinzani tu umeona chadema watu wamehama chama ili wakapate nafasi ya kugombea ubunge.
 
View attachment 3425585

Huu ndio uhalisia wa Polisi wa Tanzania?

Wakivua Sare za Polisi ndio unaona sare yake halisi.

Je, Sare ya jeshi la Polisi huwa inatumika kuhadaa Watanzania kwenye baadhi ya matukio?

Hapa ni aliyekuwa IGP Mkuu wa Mapolisi wote Nchini baada ya kuvua sare ya Polisi

Ndio maana kila siku tunapigwa Virungu vya ugoko na Polisi tena wanatupiga ili tufe sio tupone.

Saa nyingine nawaza, Ukute ni UVCCM wamevalishwa Sare za Polisi watushughulikie🤣🤣
Nchi ni Mali ya CCM ukisubiria tamko na maandishi utasubiri sana 😁😁
 
Unaelewa kama mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa ni wajumbe wa vikao vya CCM katika ngazi zao za uongozi ?

..haikupaswa kuwa hivyo.

..Ccm haina uhaba wa wanachama kufanya kazi hizo.

..kungetungwa sheria ya kuzuia wakuu wa mikoa na wilaya kushiriki shughuli za chama.

..pia wakuu wa vyombo vya ulinzi, tume ya uchaguzi, mahakama, na watumishi wa ngazi fulani katika vyombo hivyo, wangewekewa kipindi maalum cha kutojihusisha na siasa. Kwa mfano, tungeweka miaka 5 tangu waondoke katika nafasi zao.
 
Tungepata katiba mpya ingetenganisha Watendaji wa serikali na siasa za chama tawala hapo haki ingekuwepo kwenye utumishi hasa vyombo vya maamuzi kama, Police Service,Mahakama na Bunge
 
Back
Top Bottom