Mlendamboga
JF-Expert Member
- Sep 14, 2011
- 667
- 338
Aliyekuwa mbunge wa Mbozi Magharibi na baadaye jimbo hilo kubadilishwa na kuitwa Momba Miaka ya 1995-2005 Eliakim Simpasa amefariki majira ya saa 7 mchana leo hii katika hospitali ya Mkoa wa Songwe.
Simpasa ambaye aliongoza kamat ya Haki, maadili na Madaraka ya Bunge atakumbukwa namna alivyokuwa kinara wa kuita watu bungeni wakahojiwe pale walipokuwa wakijaribu kugusa mhimili wa Bunge.
Miongoni mwa walioitwa mbele ya kamati ya Simpasa kama walivyoiita watu ni pamoja na Mama Terry, Uongozi wa ITV na Radio one pale mijadala ya kipindi alichoshiriki mama Terry kugusia namna utendaji wa bunge ulivyokuwa hauwaridhishi wananchi, lakini kamati hiyo haikuridhishwa na uendeshaji wa kipindi hicho na kuwaita kuhojiwa.
Simpasa aliangushwa kwenye kiti cha ubunge na Dr Luka Siame 2005-2010, na baadaye jimbo hilo likachukuliwa na Silinde kwa vipindi viwili.
======
UPDATES:
Mwili utasafirishwa kesho trh 26~5~2020 saa 3:00 Asubuhi kutoka vwawa kuelekea Kapele, na mazishi yatakuwa keshokutwa.