TANZIA Simpasa Eliakim, Mwenyekiti wa kamati ya haki za Bunge 2000-2005 afariki dunia

Mlendamboga

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2011
Posts
667
Reaction score
338

Aliyekuwa mbunge wa Mbozi Magharibi na baadaye jimbo hilo kubadilishwa na kuitwa Momba Miaka ya 1995-2005 Eliakim Simpasa amefariki majira ya saa 7 mchana leo hii katika hospitali ya Mkoa wa Songwe.

Simpasa ambaye aliongoza kamat ya Haki, maadili na Madaraka ya Bunge atakumbukwa namna alivyokuwa kinara wa kuita watu bungeni wakahojiwe pale walipokuwa wakijaribu kugusa mhimili wa Bunge.

Miongoni mwa walioitwa mbele ya kamati ya Simpasa kama walivyoiita watu ni pamoja na Mama Terry, Uongozi wa ITV na Radio one pale mijadala ya kipindi alichoshiriki mama Terry kugusia namna utendaji wa bunge ulivyokuwa hauwaridhishi wananchi, lakini kamati hiyo haikuridhishwa na uendeshaji wa kipindi hicho na kuwaita kuhojiwa.

Simpasa aliangushwa kwenye kiti cha ubunge na Dr Luka Siame 2005-2010, na baadaye jimbo hilo likachukuliwa na Silinde kwa vipindi viwili.

======

UPDATES:

Mwili utasafirishwa kesho trh 26~5~2020 saa 3:00 Asubuhi kutoka vwawa kuelekea Kapele, na mazishi yatakuwa keshokutwa.
 
Rip Simpasa!
 
RIP hii corona kwanini inawamaliza chama tawala ?

Toka maktaba : makubwa aliyoyafanya kwa wananchi wa Momba mkoa wa Songwe Tanzania ni kuwaasa CCM kuwa maendeleo hayana chama waache kubagua !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…