Simpendi na sikumchagua Magufuli lakini naunga mkono 100% msimamo wake kuhusu Korona

Mkuu muafrika ni kuchapa viboko ndio anaenda.
 
Tanzania kuna maelfu wamekufa?

Hebu twambie basi unataka Magufuli akwambiaje kuhusu corona?
 

Mkuu inaonekana unachanganya kati ya serikali kutangaza kuwa kuna huo ugonjwa, na hatua za kuchukua. Jitahidi utenganishe kati ya kukiri uwepo wa ugonjwa, na hatua za kuchukua. Vinginevyo utabeba dhana zako kisha uishie kuwa mpotoshaji, hasa hapo unaposema tuache chuki, kanisa nalo limetoa waraka, je na wao wana hiyo chuki usemayo?
 

Kiukweli zaidi ya kuchukua tahadhari hatuna uwezo wa kuudhibiti huu ugonjwa kwa kuwaambia watu wakae ndani.

Wengi watakufa na hofu, njaa, msongo wa mawazo.

Unaitwa Novel Corona Virus for a reason. Ni ugonjwa mpya, unaobadilika. Kuna South Africa, Brazil, London na Original Chinese version.

Hata chanjo kwanza ni expensive pili hazisaidii kwa 100%. Mfano wanasema Pfizer ni 95%, inabidi zikae below minus 70% to be effective, AstraZeneca efficacy, effectiveness ni 70%. Russian is 50%.

Uwezo wa kuzalisha hizi chanjo bado ni mdogo sana duniani kukidhi mahitaji.

Bado hazijiwahi kuwa-tested kwenye sample ya kutosha to come up with, ethical, medical, serious conclusion.

Itachukua kama miaka miwili kufika Nchi maskini. Lockdown kwa miaka miwili?

Maisha lazima yaendelee.
 
Kanisa wametoa waraka wa kumalumu Magufuli kwamba kawaacha watu wafe?
 
Toa ushauri nini kifanyike ili kuondoa korona
Acha kumlalamikia mtu mmoja kwa sababu ya chuki zako binafsi
Toa njia sahihi, yeye kaona hii ndiyo nzuri watu waendelee kufanya kazi hakuna lockdown wewe unatoa ipi??
 
Tanzania kuna maelfu wamekufa?

Hebu twambia basi unataka Magufuli akwambiaje kuhusu corona?

Tatizo linakuja pale wanaosema kuna corona kukutana na vitisho vya dola. Inawezekana yeye hataki kukiri kwa sababu anazozijua, lakini serikali inapoendelea kusema hakuna corona na anayekiri hadharani kuwa ipo anakutana na vitisho, inaleta walakini. Ifahamike huo ugonjwa sio tatizo ama kosa la serikali, bali ni tatizo la dunia nzima, iweje iwe nongwa ama dhambi watu kukiri hadharani?

Wengi hatuungi mkono kuwekwa lockdown, lakini bado serikali inaweza kutangaza kurejea kwa awamu ya pili ya hivyo virus, na hatua za awali zikachukuliwa hasa fungu kutengwa ili kupambana na athari za huo ugonjwa huko mahospitalini, ama zile hela za ugonjwa toka kwa wazungu zimeliwa?
 
Mkuu tindo , kukiri bila kuwa na hatua kuna faida gani? Nadhani itakuwa ni kupandikiza hofu na panic isiyokuwa na tija.

Hamna anayepanic tena, sana sana ni watu kuambiwa wachukue tahadhari zote za huo ugonjwa. Ukimwi uko miaka mingi na watu hawapanic, ndio itakuwa hiyo corona?
 
lakini bado serikali inaweza kutangaza kurejea kwa awamu ya pili ya hivyo virus, na hatua za awali zikachukuliwa hasa fungu kutengwa ili kupambana na athari za huo ugonjwa
Hatua za awali zipi mkuu ambazo zina tija?

Na unapogusia fungu kutengwa, hili fungu litafanya kazi ipi yenye kufifisha ama kuondoa korona?

Kwa mawazo yangu itakuwa ni kupoteza muda na fedha.
 
Jiulize kwanza kwanini yeye kakimbilia Chato
Hii ni sawa na baba aliyeketi barazani jioni na familia yake kisha wote wakamuona nyoka akiingia ndani lakini kwa mshangao baba kwakuwaondolea hofu familia yake, kawaambia yule nyoka kazunguka nyumba na kutokomea zake. Watoto na mama yao wameingia ndani kwa hofu kubwa. Kwa hali isiyo ya kawaida baba yule kawaaga na kuwaambia anakwenda kutembelea mifugo yake hivyo hatakuwepo pale usiku ule. Kijijini hakuna umeme na baba kaondoka na tochi.

Hapo familia itaacha kumlaumu baba??
Je ni sahihi baba kuidanganya familia yake??
 
Wewe unataka Magufuli akufanyie nini kuhusu corona?
 
Hatua za awali zipi mkuu ambazo zina tija?

Na unapogusia fungu kutengwa, hili fungu litafanya kazi ipi yenye kufifisha ama kuondoa korona?

Kwa mawazo yangu itakuwa ni kupoteza muda na fedha.

Kila mahali kuwe na vitakasa mikono, kutokuwa na mikusanyiko isiyokuwa ya lazima nk.

Fungu lililotolewa na wazungu kwa ajili ya kupambana na Corona lingenunua vifaa tiba huko mahospitalini. Ama unataka mgonjwa akipelekwa hospitalini aachwe kisa ugonjwa huu hauna tiba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…