Simpendi nataka kuachana naye ila sijui namwachaje?

Simpendi nataka kuachana naye ila sijui namwachaje?

wenalitha

Member
Joined
Apr 24, 2016
Posts
60
Reaction score
50
Mimi ni binti wa makamo nipo na mahusiano na mtu kwa miaka mitano sasa ila tangu nimeanza nae kwa kweli sijawahi mpenda.

But nilikuwa najipa moyo kuwa nitajifunza kumpenda lakini naona jitihada zote nilizofanya ili nimpende zimeshindwa kuwork out.

Sasa shida inakuja hivi sasa tupo kwenye process za ndoa lakini ndani ya nafsi yangu naona amani inapotea juu ya hii ndoa yani nazidi kumchukia daily.Nanaona kama nikiiforce hii ndoa kwa kweli nitakuja kuwa msaliti na sitaki kuja kuishi maisha hayo.

Sasa nashindwa naanzia wapi kusema hili jambo maana ni mtu ambaye anapendwa mno na wazazi wangu sasa sijui nitaelewekaje nyumbani na sitaki kupoteza heshima na upendo niliopewa na wazazi wangu na mchungaji wangu tangu utoto wangu kwa ajili ya huyu mtu.

N.B mpaka tunaanza process za ndoa si kwamba niliridhia ila alimtumia mama yangu kama mtego wa kuninasa.
 
Ahsante kwa ushauri but sidhani kama itakuwa rahisi cause kama nilivyoeleza hapo juu ni kipenzi cha wazazi wangu.
 
Miaka yote mitano unajifunza nini mkuu?umempotezea muda wake olewa nae tu hamna namna huna huruma ata kidogo. Huyo jamaa alikua na hali ya kupendwa na MTU mwingine vizur tu.
 

Hivi unajua kipi utapitia baada ya kumuacha jamaa na kubaki akinungunika basi nakushauri usijaribu kumuacha pambana tu na hali yako vinginevyo kama utamuumiza leo basi jua kesho utaumizwa wewe na utamkumbuka huyu utakayomuacha.
 
Wanawake mna roho ngumu..yani miaka 5 unakalia dudu la mtu humpendi?!

Yani unatongozwa kwa kupitia mama yako ?..naww kupitia kwa mama yako mfikishie ujumbe kuwa humpendi
 
afu wewe ni muongo sana, kuna uzi uliutoa hapa kipindi cha nyumba ulisema wewe ni kijana wa kiume
 
Hivi unajua kipi utapitia baada ya kumuacha jamaa na kubaki akinungunika basi nakushauri usijaribu kumuacha pambana tu na hali yako vinginevyo kama utamuumiza leo basi jua kesho utaumizwa wewe na utamkumbuka huyu utakayomuacha.
It's better kuliko niolewe nianze kuwa msaliti cause kwa nionavyo hata nikiforce nikaolewa nahisi si rahisi kudumu na kama ujuavyo ndoa zetu za kikristu ni ngumu kuvunjika nami sitaki nifike huko mpaka kuja kuvunja ndoa kwa kitu ambacho naweza solve.
 
Maangamizi au masumbuko kwenye maisha yetu huanzia pale tunapojikwaa kwenye kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati sahihi......

Unapotakiwa kufanya maamuzi yanayo au yatakayo yagusa maisha yako moja kwa moja ,mtu pekee unayetakiwa kumpa kipaumbele ni WEWE kwa kiwa wewe ndio utakayekuwa muwajibikaji wa kwanza wa jambo lolote ulilolitolea maamuzi.......

Ndoa ni moja ya jambo nyeti linalokuhusu wewe binafsi na sio mtu mwingine....wewe ndio mhanga wa kwanza wa ndoa yenye migogoro na mahangaiko....wewe ndio mhanga wa. Kwanza wa ndoa iliyojaa mateso na manyanyaso wewe ndio mhanga wa kwanza wa ndoa iliyokosa furaha..........lakini yote hayo ya naweza kuzuiwa na wewe kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati muafaka......

Kwa kipindi hiki ndio unatakiwa ujue kuwa wewe ndio umeshikilia funguo na huzuni kwenye maisha yako....

Kwa kipindi hik ndio unatakiwa ujue kwanini wewe ni mtu mzima na sio mtoto tena.......

Kwa kipindi ndio unapaswa kuwaonyesha wazazi wako kuwa wewe umeshakuwa mkubwa na unatakiwa kufanya maamuzi yanayohusu maisha yako bila ya kuingiliwa......

Busara zako pekee kwenye kufanya maamuzi ndizi zitakazokuvusha salama kwenye mtego huu......

NB;

Hakuna kitu kigumu kwenye maisha kama kuishi na mtu ambaye huna furaha naye.....

Ni sawa kuishi kwenye gereza lenYe starehe za kila aina.......
 
Huyu jamaa sjui dada,ana nyuzi za nyuma anasema mara yeye ni kijana wa miaka 29 ana dem wake anashindwa kumpata,mara tena yeye ana miaka 23 anasoma udsm kuna majamaa wawil wanamchanganya,yaan huyu ana jinsia mbili,leo ke kesho me...ukiwa mwongo uwe na kumbukumbu.
 
Back
Top Bottom