Simshangai Pasco wa JF tu; hapana, nawashangaa waandishi wote wa habari popote pale mlipo nchini!

Mag3

Platinum Member
Joined
May 31, 2008
Posts
13,413
Reaction score
23,592

Huyo hapo juu ni aliyekuwa mwandishi wa habari na mwakilishi wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, mkoani Iringa, marehemu Daudi Mwangosi. Mwangosi, ambaye alikuwa pia Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC), aliuawa kwa kupigwa na bomu na kusambaratisha mwili wake wakati polisi walipokuwa wakiwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuwazuia kufungua tawi la chama hicho, katika Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi, mkoani humo, Septemba 2, 2012




Pamoja na msemaji wa Polisi mwanzoni kukanusha askari kuhusishwa kwenye tukio la hilo la kuhuzunisha, ushahidi wa picha ulikuja kutolewa ukimuonesha polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) akimlipua Mwangosi ambaye muda huo tayari anakula kichapo kutoka kwa polisi wenzake. Polisi huyo, Pasificus Cleophace Simon (23) mwenye namba G2573 alifanya mauaji hayo mbele ya wakubwa wake akiwemo aliyekuwwa Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya RPC Michael Kamuhanda.




Mke wa Marehemu, akiwa na uchungu kufuatia kifo cha mumewe akitoa heshima zake za Mwisho siku ya mazishi. Alikuwa na imani kubwa kwamba waandishi wa habari hawangemtelekeza na kwamba kuna siku ukweli ungewekwa wazi na wahusika wote nao waonje machungu kama yaliyompata yeye na wanawe kwani silaha za kujibu mapigo kwa mwenzao wanayo.



Hapo juu anaonekana Marehemu Daudi Mwangosi akihojiana na RPC Michael Kamuhanda muda mfupi kabla hajafikwa na umauti. Baadaye Michael Kamuhanda alikuja kupandishwa cheo kutoka SACP (Senior Assistant of Police) kwenda DCP (Deputy Comissioner of Police).

Sasa swali langu kwa Pasco na waandishi wote wa habari popote mliopo Tanzania, je mpo? Kama mpo vipi ile silaha yenu ya kalamu inayodaiwa kuwa kali kuliko bomu, kwa Mwangosi mmesalimu amri?
 
Last edited by a moderator:
Kuna waandishi wengine wanashangaza kweli kweli k.m. yupo huyu wa Mwananchi anaitwa Neville Meena; anaenda Marekani kutafuta kunakodaiwa kazikwa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu, Daudi Ballali, badala ya kutafuta ukweli kuhusu ugonjwa wake ulivyotokea. Ballali aliitwa Dodoma akiwa mzima kabisaa, katoka Dodoma akiwa na wasiwasi na maisha yake na ghafla huyooo anaumwa. Kaondoka kwenda Marekani kwa matibabu huku serikali ikidai haina taarifa na kudai haijui Ballali yuko wapi au kalazwa hospitali gani huko Marekani au anagharamiwa na nani...waandishi hao ambao sasa wanadai sasa kufuatilia liliko kaburi lake walikuwa wapi? Toka 2008!

Haya Daudi Mwangosi, mwanataaluma mwenzao kalipuliwa mchana kweupee na polisi chini ya usimamizi wa OCD, OCO, na RPC mwaka 2012. Msemaji wa Polisi, Advera Senso anakanusha na kudai kalipuliwa na Chadema, picha inatolewa ikionesha ukweli wa kilichotokea, akina Neville Meena kama vile hawapo, haliwahusu! Advera Senso pamoja na uongo wake wote ameendelea na wadhifa wake kama vile ni tukio tu la kawadia. Wakuu wa Polisi wote wanaohusishwa na mauaji ya wananchi wasokuwa na hatia adhabu yao ni kupandishwa vyeo! Je ni waandishi gani wanafuatilia mambo haya? Leo Mwangosi, je kesho? Meena? au yeye ana kinga maalum! Je Kibanda?
 
hes very lucky 2 top all thet skums..!!
 
Najaribu kuona Pasco anahusikaje nashindwa kabisa....au tumemgeuza punching bag humu?
 
Last edited by a moderator:
FaizaFoxy, nitavunja mwiko wangu wa kutojibizana na wapuuzi kama wewe mara hii moja tu halafu sitahangaika na wewe tena. Kwa ufahamisho, hii ndiyo ilikuwa ripoti iliyotolewa na polisi kupitia kwa msemaji wake, Advera Senso, kuhusu kulipuliwa kwa Mwangosi.

FaizaFoxy, hii ilikuwa ni ripoti iliyotolewa na Jeshi la Polisi; ni wapi unatoa ripoti ya marehemu kumvaa RPC? Wakati Mwangosi analipuliwa RPC alikuwa ndani ya gari akishuhudia na kutoa maelekezo. Endelea tu kujianika kwa kutetea ujinga...that's exactly what is expected of you.
 

Kama nimemwelewa vizuri Faiza,anasema:Marehemu Mwangosi alienda kumvaa kamanda wa kikosi cha FFU na siyo RPC kwa uelewa wangu hawa ni watu wawili tofauti au siyo Faiza?
 
@...faizafoxy ...always wewe unaleta upinzani yaani unaleta ligi hata kwenye kifo cha mwanhosi, R.I.P mwangosi hao wote waluyokufanyia unyama huo malipo dunia watayapata....watateseka na wataishi ktk hali ngumu sana washenzi wakubwa
 
Sasa swali langu kwa Pasco na waandishi wote wa habari popote mliopo Tanzania, je mpo? Kama mpo vipi ile silaha yenu ya kalamu inayodaiwa kuwa kali kuliko bomu, kwa Mwangosi mmesalimu amri?

Mkuu Mag3, kwanza asante kutukumbushia hili la Mwangosi japo kwa kiasi fulani umetonesha vidonda vya machungu yaliyopita, lakini pia sometimes ni muhimu kukumbushana ili follow up ya kinachoendelea iendelee kufuatiliwa kwa kupashana habari!.

  1. Kiukweli tukio la Mwangosi lilitugusa karibu waandishi wengi, and we did what we could do by then, lakini nakiri wazi, we didn't do enough ukiondoa zile emotions na machungu ya kifo, maandamano na rambi rambi, baada ya kuzikwa I'm not if we did much!, sijapata follow up ya mjane wake anaishije maajaliwa ya familia yake na maendeleo ya kesi, hivyo huku ni kutuamsha kama tumelala sio tuu tutimize wajibu wetu kwa jamii, pia tumtendee Daudi Mwangosi haki ili roho yake ipumzike kwa amani.
  2. Kwa upande wangu binafsi, kupitia kalamu yangu humu jf, kilichomkuta Daudi Mwangosi ni matokeo tuu, sio chanzo!. Wengi wanajikuta very emotional ku deal na matokeo lakini ni wachache wanajishughulisha na kushughulikia chanzo!. Mimi ni miongoni mwa wachache hao ambao nimedeal na chanzo hivyo naomba unifuatilia katika michango yangu hii.
  3. Historia yangu na haraka niliwahi kuiweka hapa [h=3]Miaka 50 Ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar[/h] Hivyo kutangaza police brutality sikuanza jana!.
  4. Kabla ya kilichokuta Daudi Mwangosi, niliwahi kuupandisha huu uzi humu,[h=3]Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to Know...[/h] nani aliwahi kuusoma na jee nilikuwa ninazungumzia nini?! sehemu ya uzi huo nilisema hivi
  5. Kilichomtokea Mwangosi, nilipandisha uzi huu,
  6. [h=3]IGP Mwema, Please, Please, Please, Stop This Police Brutality,[/h]sehemu ya uzi huu nilisema hivi
  7. Baada ya Polisi kumfungulia mashitaka polisi mmoja tuu, yule aliyepush the trigger, nikauliza why only him while he was following order, nikapandisha uzi huu [h=3]Waziri Nchimbi na IGP Mwema, Mnasubiri Nini Kujiuzulu? hapa nilisema hivi.
    Wale wenye kumbukumbu ya Kesi ya Mauaji Mwanza, kilichomtokea Daudi Mwangosi mikononi mwa polisi sote tumekiona, sasa nauliza hivi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Nchimbi na IGP, Saidi Mwema, mnasubiri nini kujiuzulu ili kusetiri aibu ya serikali?!.
    [/h]
  8. Waandishi wenzangu wa habari walipojidai watasusia kuandika habari za polisi kufuatia hasira ya kifo cha Daudi Mwangosi, Wa kwanza kutofautiana nao ni Maggid Mjengwa, na mimi pia niliungana na Maggid nilitofaitiana nao [h=3]Waandishi Kugomea Habari Za Kipolisi; Naomba Nichangie ..nilisema hivi,
    Wakuu mimi namsupport
    maggid, ila pia nazama deep zaidi kidogo kuliko maggid,
  9. Katika utetezi wangu kwa haki za wanyonge, sikuishia kwa polisi tuu, kwenye kutafuta haki, the most powerful person in this country kuliko hata the the president of URT ni mtu anayeitwa DPP, yeye pia sikuacha kumzungumzia!. Katika uzi huu, [h=3]DPP wetu kizuizi katika mapambano dhidi ya ufisadi - Page 2, nimesema hivi
    Sio tuu mimi na wewe hatuwezi kumbana DPP, bali hakuna yoyote mwenye uwezo wa kumbana, hata rais hawezi!.
  10. Hayo na mengine mengi ndio the most I could do as a journalist humu jf, ila pia nimefikia final stages za mwisho wa powers za mwandishi ni kuishia kuandika tuu, kupiga kelele wasikie au wasisikie hapo ndio mwisho!, nime realize, there is still a chance ya mimi kutoka kwenye kuandika na kupiga tuu kelele, na kuingia kwenye kutenda, to take actions, to act kwa vitendo, muda huo ukifika, it might be too late kwa Daudi Mwangosi lakini better late than never!.
Pasco
 

Wewe unadhani halujisalimisha? Alijisalimisha kwa kias kikubwa kwa kunyoosha mikono na bado hakusiklizwa na tatizo la huyo ni kwamba alikuwa anaandika ukweli kuhusu maovu yalokuwa yanafanywa na hao wakubwa na kwa taarifa yako alishapewa taarifa kuwa asiende huko lkn kwa sababu yeye alikuwa anatenda haki hakuona ubaya wake alienda kwenye tukio kumbe kamanda na vijana wale walikuwa na chuki binafsi ya kumuua ila wale waandishi kajanja hawakupewa adhabu hiyo.

Kwa hiyo dada yangu kumuona hapo Mwangosi sio kwamba alikuwa amemvamia kamanda Hapana ila alishajisalimisha bado hakusikilizwa akaona kuwa akienda kwa kamanda atapona kumbe yeye ndo alikuwa anaamlisha "piga tu" waandishi wao wa serikali hawakuwa na kosa kwao na hao ndo tunaowaongelea hapa na kuwakumbusha kwa nini hawamkumbuki mwenzao na hata hilo unalosema la kushitaki?

Hawashitaki kwa sababu wale viongozi wao wote wako mifukoni mwa mafisi-hadi,kwa hiyo unapaswa kuelewa dada yangu sio kukalia mambo ya siasa za Chadema na Ccm hat kwenye mambo silias kama haya. Amka dada yangu!
 
Issue ya Mwangosi tulifeli wote kama taifa hatukufanya lolote zaidi ya kulalamika tu kama mtoto aliyenyimwa pipi. Tujilaumu wenyewe. Kamanda aliyesimamia mauaji haya na cheo kapandishwa, wote tunasubiri Dr Slaa atangaze maandamano.

TUKUBALI SISI WATANZANIA KAMA JAMBO HALIJAKUTOKEA BINAFSI HATUJALI ZAIDI YA KUSIKITIKA TU: hail:

RIP Mwangosi
 
Pasco umeutendea haki uzi huu, hakika mengi umeyaeleza. Jambo nalipata hapa ni kwamba kuna uhaba wa kujua sheria, kufuatilia haki zetu na hata umaskini wa kipato kugharamikia kesi! zaidi ni pamoja na uwezo wa nani anaenda kudai haki, kwa maana ya kufungua kesi mahakamani.

Swali : Hivi chama cha waandishi haikiwezi ku file case ya mauaji ya Daudi mwangozi?
SP
 
Waandishi wa habari Tanzania wengi ni mateka wa wanasiasa, Binafsi sijawai kuona nguvu ya vyombo vyetu vya habari kufatilia na kuripoti matukio.

Vinaendeshwa kwa kufuata upepo na sio kuchimbua matukio.

Angalia kuelekea Uchaguzi mkuu unajua kabisa chombo fulani kipo mahususi kwa kumpigia debe mgombea wa kambi fulani matokea yake Mwananchi analishwa matango pori hadi siku ya Uchaguzi inafika anakua hujui sifa za mgombea anaetaka kumchagua.
 

Suala ndo hilo kwamba ni kweli hawa viongozi wa chama cha waandishi wa habari hawawezi kuitisha kesi mahakamani na watu wakaenda kutoa ushahidi? Tatizo hapa ni ukanjanja woooote hasa viongozi wao wanafanya kazi za serikali na hii ni kama tunayoona kwenye mihimili ya serikali yaan huwezi kutenganisha Bunge Mahakama na serikali kuu vyoote vinafanya kazi moja ya kuitetea serikali badala ya kusimamia taaluma zao na kuenenda na sheria,taratibu na kanuni. Na hata kwa waandishi wa habari ni hivyo hivyo hawana uwezo wa kujisimamia hivyo tusitegemee jipya hapo.

R.I.P.Mwangosi.
 
Najaribu kuona Pasco anahusikaje nashindwa kabisa....au tumemgeuza punching bag humu?

Naona kuna kampeni ya mskusudi kumrushia mawe Pasco wa JF, nina wasiwasi na baadhi ya waandishi makanjanja labda wamepunjwa mgawo wa bahasha?
 
Last edited by a moderator:
Naona kuna kampeni ya mskusudi kumrushia mawe Pasco wa JF, nina wasiwasi na baadhi ya waandishi makanjanja labda wamepunjwa mgawo wa bahasha?
Pasco anaponzwa na umaarufu wake humu ingawa sasa hivi hayuko active sana na issue za uandishi nje ya deals zake matangazo, humu binafsi nawajua waandishi wengi lakini watu wengi wanamfahamu Pasco kutokana na kuwa very active humu hasa quality ya michango yake kama mwanahabari wa muda mrefu.
 
Last edited by a moderator:
Waandishi wetu wengi wanahitaji kuonewa huruma. kwanza wengi ufahamu wao wa mambo mbalimbali ni limited sana. pili tatizo la ajira nchini linawalazimisha kuwa watumwa wa waajiri. hapo weledi wa taaluma hautumiki kabisa. katika mchanganyiko wa yote ndo maana wote wana bei kwa wanasiasa na mafisadi.

Wanaona heri ajijenge binafsi, na unapojumlisha na tishio la usalama ndo basi tena. leo hii kuna mwandishi gani mwenye ujasiri kama aliokuwa nao marehemu stan katabalo wa gazeti la mfanyakazi miaka ya mwanzo ya tisini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…