Simshangai Pasco wa JF tu; hapana, nawashangaa waandishi wote wa habari popote pale mlipo nchini!

th

Huyo hapo juu ni aliyekuwa mwandishi wa habari na mwakilishi wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, mkoani Iringa, marehemu Daudi Mwangosi. Mwangosi, ambaye alikuwa pia Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC), aliuawa kwa kupigwa na bomu na kusambaratisha mwili wake wakati polisi walipokuwa wakiwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuwazuia kufungua tawi la chama hicho, katika Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi, mkoani humo, Septemba 2, 2012

296587_4672851945587_1395901855_n.jpg

Pamoja na msemaji wa Polisi mwanzoni kukanusha askari kuhusishwa kwenye tukio la hilo la kuhuzunisha, ushahidi wa picha ulikuja kutolewa ukimuonesha polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) akimlipua Mwangosi ambaye muda huo tayari anakula kichapo kutoka kwa polisi wenzake. Polisi huyo, Pasificus Cleophace Simon (23) mwenye namba G2573 alifanya mauaji hayo mbele ya wakubwa wake akiwemo aliyekuwwa Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya RPC Michael Kamuhanda.

IMG-20120904-WA034.jpg

Mke wa Marehemu, akiwa na uchungu kufuatia kifo cha mumewe akitoa heshima zake za Mwisho siku ya mazishi. Alikuwa na imani kubwa kwamba waandishi wa habari hawangemtelekeza na kwamba kuna siku ukweli ungewekwa wazi na wahusika wote nao waonje machungu kama yaliyompata yeye na wanawe kwani silaha za kujibu mapigo kwa mwenzao wanayo.

582728_4673002029339_659749645_n.jpg

Hapo juu anaonekana Marehemu Daudi Mwangosi akihojiana na RPC Michael Kamuhanda muda mfupi kabla hajafikwa na umauti. Baadaye Michael Kamuhanda alikuja kupandishwa cheo kutoka SACP (Senior Assistant of Police) kwenda DCP (Deputy Comissioner of Police).

Sasa swali langu kwa Pasco na waandishi wote wa habari popote mliopo Tanzania, je mpo? Kama mpo vipi ile silaha yenu ya kalamu inayodaiwa kuwa kali kuliko bomu, kwa Mwangosi mmesalimu amri?
Pascal Hana haya
 
Pasco anaponzwa na umaarufu wake humu ingawa sasa hivi hayuko active sana na issue za uandishi nje ya deals zake matangazo ..........humu binafsi nawajua waandishi wengi lakini watu wengi wanamfahamu Pasco kutokana na kuwa very active humu hasa quality ya michango yake kama mwanahabari wa muda mrefu...........
Mkuu MTAZAMO , thanks for this, naomba support yako kwenye hili Wana JF, niko mbele yenu kwa unyenyekevu kuomba baraka zenu & moral support yenu jambo langu hili liwe! Mniombee Mungu asaidie, awezeshe liwe!
P
 
Waandishi wa habari Tanzania wengi ni mateka wa wanasiasa, Binafsi sijawai kuona nguvu ya vyombo vyetu vya habari kufatilia na kuripoti matukio.

Vinaendeshwa kwa kufuata upepo na sio kuchimbua matukio.

Angalia kuelekea Uchaguzi mkuu unajua kabisa chombo fulani kipo mahususi kwa kumpigia debe mgombea wa kambi fulani matokea yake Mwananchi analishwa matango pori hadi siku ya Uchaguzi inafika anakua hujui sifa za mgombea anaetaka kumchagua.
Mkuu idawa, usemayo ni kweli kabisa, naomba support yako kwenye hili Wana JF, niko mbele yenu kwa unyenyekevu kuomba baraka zenu & moral support yenu jambo langu hili liwe! Mniombee Mungu asaidie, awezeshe liwe! ili twende tukabadili mambo.
P
 
Tatizo Pascal Mayalla Hana msimamo kichwani yupo vizuri kuandika hila tatizo Akipewa Asali Kiduchu anaanza kutoka nje misingi ya Kazi yake
Mkuu BUKOBA LAND please!. Heshima kitu cha bure!. Lengo la Mungu kutuumba ni ili tulambe asali, Mama Samia anakoipeleka hii nchi ni kuwa ile nchi ya ahadi, mabomba nchi nzima yatatoa maziwa na asali hivyo kila Mtanzania atalamba na kufyonza.
Ili hili liwezekane lazima Mama asaidiwe, nimeamua kujitolea kujitokeza kusaidia, hatua ya kwanza ni kuomba sala zenu na support yenu kwangu kuniwezesha.

Hatua ya pili ni kama hao wanaotaka kusaidiwa wanautambua uwezo wako kusaidia na wanataka kweli msaada wako!, hilo sasa sio letu.
P
 
th

Huyo hapo juu ni aliyekuwa mwandishi wa habari na mwakilishi wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, mkoani Iringa, marehemu Daudi Mwangosi. Mwangosi, ambaye alikuwa pia Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC), aliuawa kwa kupigwa na bomu na kusambaratisha mwili wake wakati polisi walipokuwa wakiwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuwazuia kufungua tawi la chama hicho, katika Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi, mkoani humo, Septemba 2, 2012

296587_4672851945587_1395901855_n.jpg

Pamoja na msemaji wa Polisi mwanzoni kukanusha askari kuhusishwa kwenye tukio la hilo la kuhuzunisha, ushahidi wa picha ulikuja kutolewa ukimuonesha polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) akimlipua Mwangosi ambaye muda huo tayari anakula kichapo kutoka kwa polisi wenzake. Polisi huyo, Pasificus Cleophace Simon (23) mwenye namba G2573 alifanya mauaji hayo mbele ya wakubwa wake akiwemo aliyekuwwa Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya RPC Michael Kamuhanda.

IMG-20120904-WA034.jpg

Mke wa Marehemu, akiwa na uchungu kufuatia kifo cha mumewe akitoa heshima zake za Mwisho siku ya mazishi. Alikuwa na imani kubwa kwamba waandishi wa habari hawangemtelekeza na kwamba kuna siku ukweli ungewekwa wazi na wahusika wote nao waonje machungu kama yaliyompata yeye na wanawe kwani silaha za kujibu mapigo kwa mwenzao wanayo.

582728_4673002029339_659749645_n.jpg

Hapo juu anaonekana Marehemu Daudi Mwangosi akihojiana na RPC Michael Kamuhanda muda mfupi kabla hajafikwa na umauti. Baadaye Michael Kamuhanda alikuja kupandishwa cheo kutoka SACP (Senior Assistant of Police) kwenda DCP (Deputy Comissioner of Police).

Sasa swali langu kwa Pasco na waandishi wote wa habari popote mliopo Tanzania, je mpo? Kama mpo vipi ile silaha yenu ya kalamu inayodaiwa kuwa kali kuliko bomu, kwa Mwangosi mmesalimu amri?
Hawa wote ni waganga njaa nainapotokea mwandishi yeyote wa habari akajionyesha uwezo wake, ananyakuliwa haraka na vyombo vya habari vya kimataifa.

Tulionao ni ndondocha ambao wanatembea wameweka kakaratasi ka kijani kwenye shati incase wataandamwa kidogo. Waandishi kama Kabendela ni wachache. Mtu utatafutwa mpaka kaburi la babu mzaa babu yako lilipo kujidhihirisha wewe si mhamihaji haramu. Hi si nchi yetu tu, nchi zote zenye vinasaba vya usocialist wa china na urusi ndo walivyo. Urusi waandishi wanauawa au kufungwa vifungoni kila siku. China hiyo ni siri zao ila wanapotea au wahame nchi ndo waanike uozo wa nchi zao.
 
They killed that young man was very bad issue.

Pia kuna kipindi kila mtu anapambania nafsi yake, that you can't even write chochote.

Nchi inaanza kupata nuru, wenye uelewa wafuatilie ili ile familia kwa maana ya watoto wapate haki yao. Sijui mjane kama hajaolewa jamani
 
Tatizo la waandishi wengi tanzania wako ki maslahi fulani kulingana na upepo unakoelekea kisiasa,yaani akiona upande fulani kuna maslahi habari zake zinaelemea huko huko.
Mi naona tangu waandishi wa habari na watangazaji wa radio wapate uteuzi basi baadhi ya waandishi wameingia wivu fulani fulani ili na wao wafikiriwe yaani habari zao zinakuwa kama niza kujipendekeza/pendelea.
 
Hawa wote ni waganga njaa nainapotokea mwandishi yeyote wa habari akajionyesha uwezo wake, ananyakuliwa haraka na vyombo vya habari vya kimataifa.

Tulionao ni ndondocha ambao wanatembea wameweka kakaratasi ka kijani kwenye shati incase wataandamwa kidogo. Waandishi kama Kabendela ni wachache. Mtu utatafutwa mpaka kaburi la babu mzaa babu yako lilipo kujidhihirisha wewe si mhamihaji haramu. Hi si nchi yetu tu, nchi zote zenye vinasaba vya usocialist wa china na urusi ndo walivyo. Urusi waandishi wanauawa au kufungwa vifungoni kila siku. China hiyo ni siri zao ila wanapotea au wahame nchi ndo waanike uozo wa nchi zao.
pasko umefufuka?
 
Back
Top Bottom