Simshangai Pasco wa JF tu; hapana, nawashangaa waandishi wote wa habari popote pale mlipo nchini!

Kama nimemwelewa vizuri Faiza,anasema:Marehemu Mwangosi alienda kumvaa kamanda wa kikosi cha FFU na siyo RPC kwa uelewa wangu hawa ni watu wawili tofauti au siyo Faiza?

Hata kama ndivyo ilivyokuwa unadhani polisi walikuwa na haki ya kumuua Mwangosi?

BTW huo utetezi wa Mwangosi kumvaa kiongozi wa FFU ni upotoshaji mkubwa coz Mwangozi alikuwa anamuhoji huyo Mkuu wa FFU na sio kumvamia. Polisi waliunda zengwe ili angalau kwa 0.000001% ionekane marehemu alikuwa na kosa. Lakini hatakama marehemu angekuwa amefanya kosa kubwa kiasi gani ilitakiwa ashitakiwe na sio kuuwawa. Kwa nijuavyo mimi Polisi polisi wapo kusimamia sheria sio wao kuchukua sheria mkononi au Kutoa hukumu yakifo. Polisi hana mamlaka yakutoa hukumu.
 
Pasco yupi? Huyu ambae hana mkono? kama ni huyo yeye ni msakatonge balaa eti mayala mayala wakuzaliwa mzizima huyo si mkwele tu alianza muzilil akapewa zawadi yake kafuatia huyo msakatonge sasa yule kiongozi wao mkwele yeye atakua majivu kwenye ndege.
 
Kama nimemwelewa vizuri Faiza,anasema:Marehemu Mwangosi alienda kumvaa kamanda wa kikosi cha FFU na siyo RPC kwa uelewa wangu hawa ni watu wawili tofauti au siyo Faiza?

Hata taarifa unayoitoa ni potofu.. Wewe umeona mahali popote Mwangosi anamvaa kamanda wa FFU? Mbona wengine mnapenda kutetea ujinga na wajinga?
 
Kama nimemwelewa vizuri Faiza,anasema:Marehemu Mwangosi alienda kumvaa kamanda wa kikosi cha FFU na siyo RPC kwa uelewa wangu hawa ni watu wawili tofauti au siyo Faiza?
Na wewe unaamini hivyo? Kwamba Marehemu Mwangosi alienda kumvaa kamanda wa kikosi cha FFU? Ili iweje? mjumbe msitu, ngoja nikusaidie kidogo; bila picha kuonesha tukio, njama zilikwishapangwa na vyombo vya dola kuwabambikia kesi viongozi wa Chadema kama wahusika wakuu wa mauaji hayo. Na wapo waandishi wa habari ni kweli walishalishupalia hilo tamko la msemaji wa polisi kwamba katika harakati za kupambana na dola ni Chadema waliowatupia polisi kitu kilichosadikiwa ni bomu na kwa bahati mbaya kikamlipukia Marehemu Mwangosi.

mjumbe msitu, amini usiamini ambacho kingefuatia ni viongozi wa Chadema kukamatwa na kufunguliwa kesi ya kusababisha mauaji! Nina wasi wasi hadi leo labda wengine wao wangekuwa bado wapo jela kama si hiyo picha ikiwaonesha wauaji halisi, kikosi cha FFU. Dai kama hilo liliwahi kutolewa pale polisi walipomuuwa raia mwingine muuza magazeti mkoani Morogoro, Marehemu Ally Zona, chini ya usimamizi wa afande mwingine Faustine Shilogile siku chache tu kabla ya tukio hili la Iringa. Kama kawaida ilidaiwa ni wana Chadema waliorusha kilichasadikiwa ni risasi na kumpata Marehemu kichwani na si risasi ya moto iliyorushwa na polisi.

Hata pale bomu lilipolipuka wakati wa mkutano wa Chadema pale Arusha mwaka moja baadaye, madai yalikuwa ni hayo hayo pamoja na ukweli kuwa waliojeruhiwa na wengine kupoteza maisha ni wapenzi wa Chadema. Lakini kwa hili la Marehemu Mwangosi, polisi walikosea stepu...walitoa tamko lao kabla hata ya kujua safari hii upo ushahidi unaoonesha uovu wao. Na hapa ndipo nawalaumu waandishi wa habari; walipouawa wanaharakati walikaa kimya, wakauawa wana siasa wakakaa kimya, na walipouawa wananchi wasio na hatia wakakaa kimya, hawakujua kuna siku yatawafika wao! Cha ajabu pamoja na Nyololo kuwafungua macho, wamezidi kuficha kalamu zao!
 
Asante sana Pasco kwa maelezo murua ingawa kuna watu wanashangaa mimi kukutaja...wanauliza, kwa nini wewe na huku waandishi lukuki wamo humu! Nia yangu ilikuwa ni kufikisha tu ujumbe na nadhani japo umeweza kuwafikia wengi pamoja na hao wanaodaiwa wako humu. Naomba tu nikusahihishe kitu kimoja; ni kweli jitihada zako zilionekana humu ila mada Police Brutality in Tanzania: The World has a right to know...ilianzishwa na Mag3 tarehe 15 November, 2011 kama ifuatavyo;

[h=2]Police brutality in Tanzania, the world has a right to know![/h]
Yaonekana mods walikuja kuunganisha mada kutoka kwa watu mbali mbali...hata hivyo tuko pamoja, vitendo vya polisi nchini ni vya kulaaniwa na wapenda amani popote pale walipo. Tumeshuhudia watoto wa chekechea wakitupiwa mabomu ya machozi, akina mama waja wazito wakirushiwa mabomu ya machozi, waalimu wakitawanywa kwa mabomu ya machozi...yaani lugha ya polisi wetu ni mabomu ya machozi, maji ya kuwasha, risasi za moto; hata pale raia wema hawana hata fimbo mkononi!
 
Last edited by a moderator:
Samahani, humu ndani mimi simjui mwandishi yeyote mwingine zaidi ya Pasco...nafikiri akipata ujumbe atanisaidia kuufikisha kwa wana taaluma wenzake.

Nikipata nafasi nitakujibu kitu kupitia PM.
Je unajua kuwa kuna kesi juu ya mhusika wa tukio la mauaji? je unajua sheria inasemaje katika kujadili suala lililoko mahakamani? sijui unataka message gani itoke. kila mtu anajua kilichotokea na wahusika ni akina nani? siyo isue ya ku blame waandishi kwamba wamezembea au kitu gani,nadhani kuna tatizo la mfumo na serikali mliyoweka madarakani ambao waandishi pekee hawawezi kubadilisha hii hali,mengine pm
 

Ina maana gani basi ujibu hapa kama unahitaji kum-PM mtu mmoja tu...?si mge-pm-ana huko huko...?Uzi umewekwa hapa watu wote wajadili kuelimishana kwenye chombo chetu cha habari JF.....kuna kipi cha kuficha hapa JF ambapo hata km Rais wa nchi kadokoa hapa hatumfichi tutamuita tu ni mwizi.stand up and be counted!
 
Shughuli za jeshi la polisi zinaongozwa na sheria mbalimbali. Jeshi la polisi lina mamlaka ya kisheria na linapaswa kutumia mamlaka hayo kulingana na taratibu zilizoainishwa katika sheria husika.

Polisi wanaweza kukamata, kufanya upekuzi, kushikilia, kumpeleleza mtuhumiwa, kumhoji shahidi, kufanya mahojiano na mtuhumiwa, kutawanya waandamanaji wenye nia ovu na kuhakikisha usalama wa jamii. Wanapaswa kufanya hivyo kwa kufuata taratibu na sheria na sio vinginevyo. Polisi hawawezi kufanya wapendavyo.

Sheria zinazoongoza utendaji wa Jeshi la Polisi ni:
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai inaeleza njia ambazo polisi na mahakama wanapaswa kufuata katika kuwashughulikia wahalifu. Hii ni pamoja na mamlaka ya polisi na taratibu wanazotakiwa polisi wazifuate. Mfano mmojawapo ni matumizi ya nguvu ya polisi pale anapomkamata mtuhumiwa na nguvu za polisi anapofanya uchunguzi
Sheria ya ushahidi inaeleza kwa undani kinachokubalika mahakamani kama ushahidi. Ushahidi wowote uliopatikana kwa kutumia nguvu, hauwezi kutumika kama ushahidi halali, ikibainika mahakamani kuwa ulipatikana kwa njia batili.
Sheria ya Jeshi la Polisi namba 322 (Police and Auxiliary Services Act 2002 Cap 322).

inaeleza kuhusu uendeshaji wake, nidhamu mamlaka na kazi za polisi na mambo mengine yanayolihusu jeshi la polisi. Sheria hii inasisitiza polisi kutenda haki katika utendaji wao ili kutoa mfano wa kulinda sheria na kanuni za nchi.

Hakuna mahali ambapo sheria imehalalisha wanasiasa kuwatumia Polisi kwa malengo ya kisiasa.

Matumizi yoyote mabaya ya mamlaka au uzembe katika kazi ni utovu wa nidhamu na uhalifu. Afisa wa polisi anayetenda hayo anapaswa kuchukuliwa hatua stahiki.
 
Hapo uliposema alipigwa bomu hadi mwili wake kusambaratishwa umeandika kwa kujua au bahati mbaya?
 
Hapo uliposema alipigwa bomu hadi mwili wake kusambaratishwa umeandika kwa kujua au bahati mbaya?
Heh! Hili lako ndilo tatizo la malimbukeni wanaodandia mambo wasiyoyajua...unashangaa mwili wa marehemu Mwangosi kusambaratishwa kwa bomu! Ulizaliwa lini kijana...kumbuka JF inatunza kumbukumbu na unakaribishwa kupitia mada mbali mbali zilizowasilishwa humu siku za nyuma (naona umejiunga juzi juzi, pole sana)

Kama mods wanaruhusu, ngoja nikuwekee mabaki ya mwili wa Daud Mwangosi baada ya kuuliwa na polisi wetu wa kikosi cha FFU Iringa mwezi wa September mwaka 2012.



Kama unaitaka picha kubwa zaidi inayoonesha mwili ulivyosambaratishwa vipande vipande ni PM nitakutumia.
Kama si ushahidi wa picha, Chadema walikuwa wameshabambikiziwa kesi ya kuua (kumlipua mwandishi kwa bomu)
Hatun Jeshi la Polisi, tunalo genge la wauaji!​
 
Nilitegemea ujibu kutokana na swali, kuwa una hakika au umeandika bahati mbaya ila cha kushangaza umeanza kwa kunishambulia japo mi huwa sina kinyongo na watu kama wewe.

Hapo kwenye picha askari wanaonekana wame-concentate na kitu kingine kabisa na sio hayo mabaki, nitafsirie hapo maana ni kama hawayaoni (hakuna mabaki)

Pia nitumie tu hiyo picha nyingine na ukimaliza nami nitakwambia nilishiriki vipi hadi kuchimba kaburi lake na kuaga mwili.
 
Mtoa post acha ukuda, kama hoja ni kuuliwa basi wazanzibar walishauliwa sana miaka ya nyuma hadi leo na cjakusikia kusema chochote, sasa ni zamu yenu watanganyika kulinywesha jini ccm damu ya watanganyika acha kulalamika.
  1. Historia yangu na haraka niliwahi kuiweka hapa [h=3]Miaka 50 Ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar[/h] Hivyo kutangaza police brutality sikuanza jana!.
Natumaini, umenipata.
Paskali
 
Wanabodi,
Leo ni siku ya kimataifa ya uhuru wa habari, kila mwaka sisi waandishi huwa tunakutana mahali kwa siku 2 na kujadili mambo mbalimbali kuhusu uhuru wa habari, na katika mkusanyiko huo, serikali, vyama vya habari na Taasisi za habari hutoa matamko kede kede kuhusu uhuru wa habari, lakini kwa mwaka huu, kufuatia janga la Corona, hakuna maadhimisho yoyote rasmi ya kukutana, ila nilitegemea wizara ya habari, vyama vya habari na mashirika na Taasisi za habari zitoe matamko mbalimbali.

Bado sijabahatika kuona tamko lolote!, ila usikute zile speech huwa zinaandaliwa kwa ajili ya presentations kwenye kongamano hotelini, safari na per diem!, leo hakuna safari, no trip, no per diem, no hotel gathering, hivyo this time hata speech tuu hakuna?!.

Nawatakia waandishi wenzangu, maadhimisho haya ya kimya kimya, nawashauri wale wafadhili mbalimbali wa tukio hili, kwa vile hatukusafiri, wala kula na kulala hotelini, then naomba hao wafadhili watutumie tuu hizo per diem, tutahama majumbani mwetu na kuhamia hotelini 3 days kisha tutatoa matamko.

Paskali
 
Muulize kwanini mke wa askari aliyehukumiwa kwa mauaji ya mwangosi alipatiwa ajira kujikimu na maisha kwakuwa mumewe yupo jela na mke wa mwangosi hajapatiwa ajira
 
Sasa swali langu kwa Pasco na waandishi wote wa habari popote mliopo Tanzania, je mpo? Kama mpo vipi ile silaha yenu ya kalamu inayodaiwa kuwa kali kuliko bomu, kwa Mwangosi mmesalimu amri?​
Mkuu Mag3, the pen is mightier than the sword kwa nchi ambazo jamii kubwa ni literates wanasoma maandishi, lakini kwa jamii iliterate kama yetu, the pen doesn't matter much, hivyo baada ya kuwa a pen pusher for more than 30 years, nimegundua pen doesn't matter much, hivyo sasa nimeamua mazima ndani ya ngoma tuicheze na kuleta mabandiko from within.
Hivyo kuna hili jambo langu naomba uungwaji mkono wako lifanikiwe niingie mitaa hii nikasaidie kutokea huku
P
 
. leo hii kuna mwandishi gani mwenye ujasiri kama aliokuwa nao marehemu stan katabalo wa gazeti la mfanyakazi miaka ya mwanzo ya tisini?
Mkuu Grand Jury, waandishi wenye ujasiri huo kama wa Stan Katabalo, tupo, ila zama zimebadilika, kila zama na zama zake!. Kama sisi waandishi wote wa habari wenye ujasiri kama wa Stan Katabalo na wote tukafanya kama Stan, nani angebaki kuuliza maswali kama yale ya Kiti Moto?. Waandishi wa Habari na Kupotea/Vifo vya Kutatanisha, Toka Katabalo, Saanane, Gwanda, Mwangosi, Isango. Ni Ama Tuombe Mungu Atunusuru ama... wengine tumechagua ile ama ya pili ndio maana leo tupo!.
Paskali
 
Kwahiyo wewe ni mwandishi wa habari mwoga!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…