Simu inapokuwa sisimua!!!

KakaKiiza

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2010
Posts
11,794
Reaction score
9,075
Wadau jamani hapa kuna tatizoo!!
Hivi naomba kuwekwa sawa katika hili jambo kwani nafahamu mambo haya kwenye jamii yanajirudia lakini inategemea ni wakati gani na mazingira yapi!,Mpenzi wangu anataka kila simu inayopigwa afahamu SMS aisome!! nikisema kila mmoja ana simu yake hivyo haifai kufatiliana kwenye simu ya mwenziye anasema je Una love afair nje zaidi yangu??Nimeweka securty code anataka ajue code yake!! hapo ndo ugonvi unapokuja kisa eti kama mimi nimpenzi wake kwanini nifiche??nakwanini niweke securty code??yeye eti kwanini afichi??Je hiyo ni halali kunyanyaswa kwenye simu yangu?Kwanini kila mmoja asikae na simu yake?kwanini utafute shari kwenye simu ya mwenziyo eti nyie wabeijing nini jamani??:A S 39:??
 
mwanamke ana matatizo na wewe pia .....

kwani lazima na wewe ufiche? trust me ukiwa hufichi ataacha kukuuliza............na pia kama unataka uache kuulizwa msg zinatoka wapi, zile msg za muhimu uwe unamuambia zinasemaje kabla yeye kukuuliza.
 
kakakiiza, kwnai kuna unaloficha kwenye hiyo simu yako? ni kweli kuchunguza simu ya mwenzi wako haipendezi lakini kama simu hiyo ikiwa protected sana hata mi nitataka kujua kuna nini kinachofichwa huko. be free na simu yako then utaona kama atakuwa na sababu ya kuchunguza!
 
Huyo mwanamke anahisia kali kwamba kuna kitu inaendelea. Anaweza kuwa sahihi au anakosea. Kwa hiyo ni jukumu lako kuonesha kuwa yuko sahihi au anakosea. Mpe simu achezee kama toy uone kama kutakuwa na swali tena. Ila ukizidi kuficha ndo unauwasha zaidi.

Pamoja na kumpa uhuru wa kuchunguza simu yako anavyotaka, mweleze tu kuwa siyo vizuri kukufanyia ushushu usio na maana kiasi hicho. Na kwamba unahitaji uhuru kiasi fulani ingawa usidai uhuru 100%. Kitu hicho hakipo kwenye ndoa.
 
Kama unajiamini uko safi mpe ahangaike nayo ikimchosha atakurudishia . lakini kama hujiamini ndo hapo sasa :lie:
Tena mwambie ya kwake akupe wewe ili utumie katika kipindi akiwa na ya kwako ..
 
Kama unajiamini uko safi mpe ahangaike nayo ikimchosha atakurudishia . lakini kama hujiamini ndo hapo sasa :lie:
Tena mwambie ya kwake akupe wewe ili utumie katika kipindi akiwa na ya kwako ..

Ninafanya hayo yote lini ukishampa ujiandae kutafuta new contact kwani majina ya mwajuma,havijawa sikitu,mwatakaje Hautayakuta kamwe ndio maana naweka securty code kuprotect contact zanu lakini yeye hataki mimi nitumie hiyo huduma!!
 
Kama unajiamini uko safi mpe ahangaike nayo ikimchosha atakurudishia . lakini kama hujiamini ndo hapo sasa :lie:
Tena mwambie ya kwake akupe wewe ili utumie katika kipindi akiwa na ya kwako ..

Sure,

Watu wengine wanajitakia matatizo. Kama analilia simu, si ampatie tu. Kung'ang'ania kuificha kunazidisha wasi wasi. Mimi simu yangu iko huru kuguswa wakati wote kama bidhaa za wamachinga. Namna hiyo vuvuzela zitatoka wapi?
 
so simple
1.km kweli hakuna kibaya kwanini ufche simu yako km bomu??????frankly spkng ma brooo km akuna kibaya chochote na unajiamin kwanini umfiche???? yes i knw its against human rigt cz kila mtu anatakiwa awe na privac zake bt km unampenda mwenzako na cm inamtia kiwewe y shouldnt u gve ha da fone??
- ninachokiona kwako ni UNA CHEMBE ZA HATARI km hauna wasi wasi kwanini uweke code ?km ukiweka kwa sababau nyngine stl unaweza kumpa code pia ye akaijua.....??
-anataman sana simu yakko cz kuweka code na kumwambia kila mtu na cm yake ndicho kitu kinamtia mashaka!

km ungempa uhuru wa kushika cm ako wala yani asingekuwwa anachachawa na cm ako na aman ingekuwa A
advce:
to a code apate uhuru wa kuchek cm ako
km una madudu acha
 
mwanamke ana matatizo na wewe pia .....

kwani lazima na wewe ufiche? trust me ukiwa hufichi ataacha kukuuliza............na pia kama unataka uache kuulizwa msg zinatoka wapi, zile msg za muhimu uwe unamuambia zinasemaje kabla yeye kukuuliza.
Nafikiri kuna mambo ambayo huwa ni ya binafsi zaidi. Unaweza kuwa una mambo mhimu ambayo unawasiliana na wazazi wako au kuna jamaa zako ambao mnafanya nao mambo ambayo si lazima mkeo ajue, sasa kama kila simu itakayopigwa na msg itakayoingia anataka na yeye asikie au asome ina maana sababu ya kuwa na simu ya kiganjani ni nini? Si bora kununua TTCL ya mezani? Kwa mfano ofisini huwa kuna siri nyingi na za aina tofauti tofauti. Kuna ambazo unaweza kushare na mkeo au mmeo kuna nyingine huwezi. Sasa kama akikagua simu yako akaziona itakuwaje? Nafikiri ni vizuri kuwe na mipaka ya uhuru katika simu.
 
Simu ni mali halali ya mtu anayeimiliki. (Nashukuru wazo la kuzisajili lilibuniwa) Ana uhuru wa kumpa mtu mwingine aitumie au laa. Hakuna mtu yeyote mwenye mamlaka ya kunilazimisha atumie simu yangu au aangalie kilichoandikwa kwenye simu yangu. Hamna mwenye mamlaka ya kujua nimempigia nani au nani kanipigia. Mi siipekui simu ya mke wangu naye ni marufuku pia kuipekua simu yangu bila idhini yangu....Period!!:closed_2:
 

:A S tongue::A S tongue::A S tongue::A S tongue::A S tongue::A S tongue:
kumekucha
 

Kwa shari au amani? It sounds evil!

Hatuongelei kupekua. Tunaongelea kuwekeana vikwazo na mipaka isyo na msingi. Pia hatuongelei mtu yeyote hapa. Tunaongelea mke au mume. Hata hivyo kila ndoa ni "Taifa huru" (sovereign state) na kama wote mnakubalina na hali hiyo hakuna neno. Tatizo ni pake ambapo kila mmoja anahisi hatendewi haki kama kwenye hii story. Dawa yake ni kuweka codes?
 
Sure,

Watu wengine wanajitakia matatizo. Kama analilia simu, si ampatie tu. Kung'ang'ania kuificha kunazidisha wasi wasi. Mimi simu yangu iko huru kuguswa wakati wote kama bidhaa za wamachinga. Namna hiyo vuvuzela zitatoka wapi?

Umenichekesha sana DC na hiyo sentesi yako hahahahahaah
 

:A S tongue::A S tongue::A S tongue::A S tongue::A S tongue::A S tongue:
kumekucha

Karibu mkuu. Wewe umeshaweka codes?

Nashauri hata kule vyumbani pia tuweke codes. Ila mpwa, kuna msg unakutana nayo kwenye simu ya my wife unatamani kufa!! Inataka moyo lakini, ingawa ni bora tu kujua kama unaishi na mtu au panya kwenye debe la unga!!
 

Mi simu yangu inawekwa security code siku hiyo hiyo iliponunuliwa.
 
Umenichekesha sana DC na hiyo sentesi yako hahahahahaah

Uwe na amani na siku njema. Naamini ukicheka kidogo tu, hata malaika wa mbinguni wanafurahi pia! Siyo vizuri kwenye maisha kuwekana roho juu.

Ila siku ukikutana na kigongo kwenye simu ya mr/mrs ndo unalijua jiji! Labda siku nyingi tuanzishe mada ya kama ni vema kujua au kutojua!!
 
Mi simu yangu inawekwa security code siku hiyo hiyo iliponunuliwa.

Kama mke wako anaona sawa hakuna neno. Ila ukikwazika akaleta mada tutamshauri na kumpatia uzoefu wa upande mwingine. Yaani sisi wengine tusiojua kitu kinachitwa codes na unnecessary privacy kwenye ndoa!
 

Ndiyo kwa mustakabali huo na kwa faida ya afya zetu zimu zinalazimika kula sekyurite kodi. Nani afe na mapresha kwa umri huu wakati SBL imeongeza uzalishaji wa Serengeti?:twitch:
 

Ya nini Malumbano??...:A S confused:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…