Simu ya mwenza wako ya nini? Unajipa presha bure

Kama huna chochote kibaya kwa nini uwe na wasi wasi na simu yako... Mwenza akichukua simu yako kuangalia muache tu, shida ipo wapi...

Ila kuna tabia siyo nzuri... Zile za simu ya mwenza wako ikiita ushasimamisha shingo na kutega masikia kujua nini hicho... Sms ikiingia ushatoa macho...


Cc: mahondaw
 
Kuwa na wasiwasi inamaanisha tayari kuna mabaya mkuu.
 

Duhhhhhhhhhhh!!!
Owkey..
 

Duhhhhhhhhhhh!!!
Owkey..
 
MIMI NILIDHANI UNDESEMA ACHANA NA MWENZA, SIMU YAKE NA HUYO MPENZI WAKE WAENDELEE. MIMI NI JASIRI NIMEFANYA HIVYO. MVUA INANYESHA HALAFU UNASEMA HAKUNA MVUA NI JUA HILO KISHA UNAJIAMINISHA KUWA HAINYESHI NA MITO INAJAA UPO HAPOHAPO! KWELI?
 
Kichwa chako kizima sana. kinafanya kazi vizuri sana
 
Kuna rafiki yangu mmoja hivi hajatulia kivile kwa wanawake, sasa akawa anahisi mke wake ana cheat na huyo mke wake ni kutoka nchi jirani sema ni mjanja mjanja sana. Basi sijui nani alimpa ushauri wa kwamba afanye kila njia a hack simu ya mke wake ili kujua njema inayo toka naye.

Jamaa ana vijipesa akajaribu kucheki na jamaa wa kampuni moja ya mawasiliano kama wanaweza msaidia ikashidikana, sasa wazo likawa ni kutafuta app za phone spy, akapata moja kwa USD 80 akalipia kwa Mastercard, akatumiwa link ya kupakua appl na ilikuwa ni ya kuisntall kwenye device mbili, au simu mbili.

Mpango wa kuinstall kwenye simu ya mke wake ukaanza make lazima upate simu ya mtu unaye taka ku mspay na uinstall, jamaa katumia trick ya kwamba simu yake imekufa na kuna email muhimu ya kazini so akapewa simu ili asome email kumbe ndio kufanya instalation.Baada ya hapo sasa ni kuanza kufuatilia, ila jamaa ni mtu wasafari sana sasa akampatia mshikaji wake mmoja laptop na jukumu la kufuatilia kila kinacho toka kwenye simu ya mke wake, make app ilikuwa ina track call, picha, sms, whatsapp, facebook mesenger, Insta na hata twiter. Rafiki yake ile siku ya kwanza tu alicho kuiona, akakataa kyendelea na zoezi akazuga amepata dharura, ikibidi sasa jamaa arudi safari aje mwenyewe asome na kufuatilia simu.

Jamaa amerudi ile amelog in na kuanza kuangalia, jamaa kidogo azimie kwa alicho kiona, jamaa anakuambia yeye mwenyewe anapenda wanawake ila alicho kishuhudia kilimtisha sana, sema jamaa alijipa ujasiri akaendelea kufuatilia kwa mwezi mzima make app ilikuwa ni ya mwezi mzima.

Kwenye device ya pili nayo akainstall kwenye simu ya mchepuko wake mwingine ili aangalie kama anaweza replace mke wake,huko kwenye mchepuko nako akukatana na yale yale kama ya kwa mke wake,mshikaji anakuambia wanawake wanatongozwa sana facebook huko ndiko wanako gawa number,yaani Instagram na facebook huko sio salama kabisa, make mshikaji alikutana na jam ya watu wanaomba number na wanatumiwa, wengine wanapotezewa.

Ninavyo andika jamaa walisha gawana mbao na huyo mke wake kitambo sasa, jamaa aligoma kuvumilia akaamua kila mtu afuate mambo yake.

Mshikaji ila anajutiaga sana anasema bora asingefuatilia,make anasema anaona kama wanawake wote wako sawa sawa tu kwa tabia.Sema kavuta mwingine ila amekoma kufuatilia mawasiliano ya simu ya mke wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…