Traxtion
JF-Expert Member
- Dec 10, 2021
- 8,000
- 16,414
Nimeona leo tangazo la simu za Raddy ambazo zinatengenezwa Tanzania. Ni hatua nzuri na nimefurahi kuona simu hizi za hapahapa Tz, maana wanasema kiwanda kimeajiri watz zaidi ya 1000 ila natamani wangeimprove product zao
Kwa mfano nimeona hii simu yao inaitwa "Raddy Janja Pro" inauzwa 350,000/= na inakuja na Android 14 toleo la miaka mitatu nyuma, storage 128, battery 5000mAh lakini jina la processor hakuna, na specifications za camera haziko clear. Ni dhahiri watakuwa wanatumia processor za zamani weak sana kiasi kwamba wameona aibu kuweka jina lake
Simu kama Samsung Galaxy A17 ambayo inakuja na chipset ya Exynos 1330, same storage na battery size, specifications za kamera za kueleweka, design nzuri na bei reasonable, Android 15 na miaka 6 ya updates inauzwa bei sawa na hii ya Tz, kwa hiyo hizi simu za nyumbani zinakuwa ziko way behind competition.
.
.
Kwa sababu ni kiwanda cha kwanza cha aina yake Tanzania, ningeshauri serikali kuinvest hela kwenye kiwanda hiki, na ikiwezekana kuwashushia kodi iwezekanavyo, kuwarahisishia access na raw materials kama ikiwezekana ili kampuni ianze kutengeneza simu nzuri kwa bei nzuri yenye teknolojia mpya ili ziendane na competition kutoka nje na kusaidia kampuni iwe na foundation nzuri ili isiendelee ku produce crappy priducts ikajifia mbeleni
Kama kampuni ikashirikiana na serikali kwa miaka 5 ya mwanzo kujenga brand na foundation nzuri inakuwa rahisi kuanza kupanda kutengeneza simu za juu zaidi, kufikia level za midrange na hata flagship miaka ya mbeleni na kuanza kuuza hata nchi za jirani za Africa. Haya ndio mawazo yangu, coz wakianza kutengeneza crappy products watu watazipuuzia miaka ya mbeleni na hofu yangu kampuni itajifia wakati ndio kwanza tumepata kampuni ya kwanza inayotengeneza simu
They have to do better. Watengeneze simu nzuri kwa bei rahisi kama Xiaomi ilivyoanzaga miaka ya 2010s, ni heri waanze vizuri ili hata wakiangalia miaka 10 ijayo waone watakuwa wamepiga hatua, sio miaka 10 ijayo kiwanda kilifungwa, au tuliwauzia wachina
Hata Nothing Phones zimeanza kutengenezwa juzijuzi tu ila hawakuanza kutengeneza low quality phones, walikuja na mwanzo mzuri na ndio inawasaidia kukua