nameless girl
JF-Expert Member
- Apr 22, 2012
- 4,195
- 2,678
2008 kipindi nipo kidato cha tano, nilitokea kuwa na rafiki wa kiume ambaye tuliheshimiana kama dada na kaka. Wakati nikiwa rafiki wa kijana huyo, pia nilikuwa na shoga yangu ambapo wote watatu tulikuwa darasa moja, jambo lililopelekea wote watatu kuwa marafiki sana.Baada ya kumaliza kidato cha sita, urafiki wangu na kijana huyo ulikuwa wa karibu zaidi kuliko nilivyokuwa na shoga yangu. Baada ya siku kadhaa, kijana huyu alinieleza ukweli kuwa yeye na shoga yangu walikuwa wapenzi toka kidato cha tano. Kiasi taarifa hizo zilinishtua kidogo kutokana na kunificha ingawa wote watatu tulikua na ukaribu wa kuambiana lolote. Baada ya kuniambia hayo, kijana huyu aliniomba twende nje kidogo ya mji tukae angalau kwa siku mbili. Sikuona ubaya wowote kwani ni mara nyingi tulizoea kwenda sehemu mbalimbali. Tatizo lililoibuka ni kuwa huyu kijana alitaka tukae chumba kimoja kwa siku mbili na nisimwambie mpenzi wake (shoga yangu). Kiukweli sikuweza kwenda kwani sikujisikia amani yoyote kufanya hivyo. Sehemu zote tulizotoka, ilikuwa ni siku moja na hata mpenzi wake nilikuwa nikimjulisha kuwa tupo sehemu fulani (kipindi hiko sikuwa najua kama ni wapenzi mpaka kijana huyo aliponijulisha mwenyewe) nilijaribu kumwelewesha athari za kufanya hivyo lakini alikimbilia kunieleza kwamba hakuwa ananitamani au kunipenda kama nilivyofikiria ingawa sikuwa nimefika huko kinachonishangaza ni kijana huyu kunikwepa mara tu nilipoonyesha kumkatalia alilolitaka, hapokei simu yangu yoyote na wala hanijulii hali kama ilivyokuwa mwanzo. Mimi binafsi nampenda kama rafiki yangu wa kawaida na sipendi mimi kuwa chanzo cha ugomvi wao katika mapenzi yao. Sijamweleza shoga yangu haya yote na mpaka leo ni rafiki yangu wa karibu. Simwelewi kabisa huyu mtu. s